Wakati Real wakifunga virago jana ndugu zao
Barcelona leo watakuwa na kibarua kizito mbele ya Bayern Munich baada ya
kunyukwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza na kutoa uwezekano wa
kuchezwa fainali ya kwanza inayowakutanisha Wajerumani pekee.
Mshambuliaji Karim Benzema aliingia akitokea
benchi na kuifungia Real bao la kwanza katika dakika 82 akimalizia pasi
ya Mesut Ozil kabla ya Sergio Ramos kupachika bao la pili kwa shuti la
karibu baada ya kupokea pasi ya Benzema.
Real watajilaumu wenyewe baada ya washambuliaji Cristiano Ronaldo, Gonzalo Higuain na Ozil kupoteza nafasi tatu za wazi za kufunga wakiwa wao na kipa Dortmund, Roman Weidenfeller.
Real watajilaumu wenyewe baada ya washambuliaji Cristiano Ronaldo, Gonzalo Higuain na Ozil kupoteza nafasi tatu za wazi za kufunga wakiwa wao na kipa Dortmund, Roman Weidenfeller.
Dortmund walipata pigo katika dakika15 baada ya
kiungo wake Mario Gotze kuumia na kutoka nje nafasi yake kuchuliwa na
Kevin Grosskreut.
Utamu wa mchezo huo ilikuwa ni vita baina ya beki
wa Real, Ramos na mshambuliaji Robert Lewandowski wa Dortmund aliyeweka
rekodi ya kufunga mabao nne katika mechi moja ya nusu fainali ya Ligi ya
Mabingwa wiki iliyopita.
Katika dakika 48, Lewandowski alikosa bao baada ya
shuti lake kugonga mwamba na kurudi uwanjani, kipa wa Real, Diego Lopez
alifanya kazi nzuri kwa kuokoa mashuti ya Reus na Pisczek katika dakika
ya 61 na 64.
Kocha Jose Mourinho aliwapumzisha Fabio Coentrao,
Gonzalo Higuain na Xabi Alonso na kuwaingiza Karim Benzema, Kaka na
Sami Khedira waliobadiliko mchezo wote kabisa kwa wenyeji.
MUUJIZA
Barcelona wanahitaji mzuka wa Deportivo La Coruna kuweza kubadilisha matokeo ya mabao 4-0 waliyofungwa na Bayern Munich leo watakapokuwa nyumbani katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa.Deportivo La Coruna iliwashangaza wengi kwenye michuano hiyo msimu wa 2003-04, wakati walipoichakaza AC Milan 4-0 katika mchezo wa marudiano na kuwafungasha virago kwa jumla ya mabao 5-4.

Mshambuliaji wa Uruguay, Walter Pandiani alifunga
bao la kwanza katika dakika tano kwenye usiku ya kumbukumbu uwanja wa
Riazor, wakati La Coruna ilipoiduwaza Milan iliyokuwa na nyota kama
Paolo Maldini, Kaka na Andriy Shevchenko.
Pandiani anaamini Barca pia inahitaji bao la mapema kama kweli wanataka kucheza fainali jijini London kwenye Uwanja wa Wembley.
“Kufunga bao la mapema katika mechi ni hatua muhimu ya kuwafanya wachezaji kujiamini zaidi,” alisema Pandiani.