Simba:Ngasa hatusumbui kichwa

Baada ya siku mbili tu kupita tangu winga wa Simba, Mrisho Ngasa ajiunge Yanga, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage amesema kuondoka kwa mchezaji huyo hakuwasumbui hata kidogo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Ngassa alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, klabu aliyoichezea kabla ya kujiunga na Azam FC na kisha kutua Simba alikocheza msimu mmoja uliomalizika wiki iliyopita.
Simba wanadai Ngassa alikuwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kwao, kabla ya kusaidi wa Yanga jambo linalizua utata kwenye klabu hizo mbili kongwe nchini.
Akizungumza kwa simu jana, Rage alisema haipo sababu ya kuumiza vichwa kuhusu Ngassa kwani sheria za usajili ziko wazi na kufahamika kwa kila mtu.
“Sheria ziko wazi, hatuna sababu za kuumiza kichwa. Kwa sasa tunajipanga kufanya usajili siyo tena kufuatilia mambo ya Ngassa,” alisema Rage.
“Hatuwezi kila siku kukaa na kuzozana kuhusu sheria...Ngassa hawezi kutuumiza kichwa, tuna mambo mengi ya kufanya ikiwa kujipanga kwa ajili ya usajili.
“Sheria ziko wazi na mkataba wake na sisi upo TFF, hivyo muda utakapofika kila kitu kitawekwa wazi,” alisema Rage kwa kujiamini.
Aidha, Khalfan Ngasa ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji Ngassa amewataka mashabiki wa soka hususan wale wa Simba wasimchukie mwanae kutokana na uamuzi wake wa kurejea Yanga.
Akizungumza na Mwananchi, Khalfan alisema kuwa uamuzo kuhama timu moja na kujiunga na nyingine ni kitu cha kawaida, hivyo mashabiki Simba wasichukulie kama ni usaliti.
“Nadhani tuheshimu uamuzi wake kwasababu katika soka hilo ni jambo la kawaida kuhama timu moja na kwenda nyingine na ndiyo maana alitoa Yanga, akaenda Azam, Simba na sasa ameamua kurudi Yanga.
“Yule ni mtu mzima hata mimi siwezi kumpangia mambo yake, sana sana kama baba yake kazi yangu ni kuhakikisha anapata haki zake kama kawaida,”. alisema Ngassa ambaye ni kocha wa timu ya Polisi Iringa.
Katika hatua nyingine uongozi wa Simba umesema umepangwa kutumia kiasi cha dola za Sh40 milioni katika ujenzi wa uwanja wao ulipo Boko nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Angalia ww rage mambo ya mwaka jana mctuletee maana hamchelew mara twite cjui yondan mwisho ilikuwaje?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad