Taarifa ya Jeshi la Polisi Kukanusha Taarifa ya gazeti la Jamhuri Kuhusu Muuaji wa Kamanda Barlow

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu “MKUUPOLISI” Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,

Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.


28 MAY, 2013


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI


Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27 Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83, yenye kichwa cha habari “MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW”.

Taarifa hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na ugonjwa wake wa akili.

Jeshi la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye lengo la kupotosha jamii.

Imetolewa na:-

Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Don't trust Police Force. They are top crimminals.

    ReplyDelete
  2. duuh! hii ndo Tanzaniano.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad