Kwa sasa hali ya kawaida inaanza kurudi. Vyombo vya usalama vinaendelea kuchunguza ili kujua mlipuko huo ni nini hasa.
Balozi wa papa nchini na viongozi wa juu wa jimbo wameondoka eneo la
tukio salama na balozi hajadhurika kabisa ingawa mlipuko huo ulilipuka
karibu nao.
Mkuu wa mkoa alikuja na sasa ameondoka.
Wananchi wameanza kupungua eneo la tukio na wengi wanaelekea Mount Meru
ili kuwatambua majeruhi. Hivyo idadi ya watu wanaondoka eneo la tukio na
kwenda hospitali.
Polisi wamekamata pikipiki ambayo inasadikiwa imetumika katika tukio hilo.
Shughuli ya uzinduzi wa kanisa hilo imeahirishwa hadi tarehe ambayo haijatajwa
Mungu awajalie majeruhi wapate nafuu haraka.
wakristo tumekuwa kimya sana,uu ni upuuzi wanaoufanya hawa watu,mwisho wake tutashindwa hata kuja kutembelewa na wageni kwa ujinga wa watu wachache wanaojifanya wanipenda sana dini yao na dini yao ndiyo ya maana sana
ReplyDeletewatangaze kuna ugaidi kama walivyofanya lilipotokea tukio la zanzibar, kumbe na nyinyi mnapenda kutembelewa na wageni
ReplyDelete