Updates: Yaliyojiri Mtwara Leo- hali bado tete (Mei 23, 2013)

   
    Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
    Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
    Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
    RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
    Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
    Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
    Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.



    Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.



    Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.



    Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote



    Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.



Update: Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.

Update:

    Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
    Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
    Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.



Update:

    Mwanamke anayekadiriwa miaka 25 mjamzito auawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.

Source:Jamii Forums

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nguvu nyingi za nini? Tutumie Maneno ya Busara

    ReplyDelete
  2. Hakuna hata maneno ya busara yanayoweza kusaidia hao chinga wangekua na busara wasinge yafanya hayo waliyo yafanya mpaka kupoteza maisha ya watu wasio na hatia.Kwa kuchoma nyumba na kupora mali za watu ndio suluhisho la gas kubaki mtwara wa chochezi wa vurugu hizo wapo wamekaa pembeni wanakula bata na familia zao sisi tusio kuwa na busara ndio tunamalizana wenyewe ukichoma duka moto,shule,hospitali huduma utapata wapi?kama sio tunajitesa wenyewe nakujirudisha nyuma kimaendeleo.

    ReplyDelete
  3. Si ndo hapo ndg,maguvu ya nini? Ukiona hivyo kuna jambo wanaficha,mijitu hii imetuchosha kwakweli

    ReplyDelete
  4. Hivi serekali yetu haina njia za nyingne ya kutuliza ghasia ni mpaka watumie mabomu na kuuwa watu ndio njia sahihi? Tumieni busara kuzungumza na hawa watu watawaelewa tu, hii inaonyesha ni jinsi gani haumjiamini thuswhy mnabakia kutumia ubabe kufunika mambo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad