Winga wa Azam, Uhuru Selemani mwishoni mwa wiki
aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook akitaka wadau wamsaidie
kutafuta timu ya kwenda kucheza msimu ujao.
Uhuru aliandika “Leo Mei 24 nimetimiza miezi sita
tangu nilipotua Azam, naomba mnisaidie nienda wapi Coastal Union, Simba
au Azam.”
Naye mshambuliaji wa Kagera Sugar, Themi Felix
alisema mkataba wake umemalizika na kutoa nafasi kwa klabu ambazo
zimevutiwa na kiwango chake ili zumsajili.
“Nimemaliza mkataba na Kagera. Kwa hiyo ninafikiri
ni muda mwafaka kwa timu ambazo zilivutiwa na kiwango changu
kunisajili,”alisema Felix.
Wakati huohuo, beki wa Azam FC, Said Mourad
aliliambia Mwananchi kuwa mkataba wake unakaribia kumalizika na yuko
tayari kujiunga na timu nyingine.
“Mkataba wangu na Azam unakaribia kumalizika. Kwa
sasa imebakia miezi kadhaa kabla ya kufika kikomo. Kwa hiyo kama kuna
timu inataka kunisajili ninakaribisha mazungumzo,” alisema beki huyo.
Pia, wachezaji wa Simba, Ngalema Paul na Abdallah Juma wameamua kukatisha mikataba yao ya kuitumikia klabu hiyo.
Ngalema alisema ameamua kusitisha mkataba huo
kutokana na chuki zinazoendelea baina yake na viongozi wa klabu hivyo na
ameona hawezi kuendelea kuitumikia klabu hiyo zaidi ya kuangalia
ustaarabu mwingine.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’ire ‘Mzee
Kinesi’ amethibitisha kupokea barua za wachezaji hao kusitisha mikataba
yao ndani ya klabu ya Simba, ambapo Ngalema alikuwa amebakisha miaka
miwili wakati Juma mkataba wake ukimalizika Desemba mwaka huu.
Wachezaji wengine ambao mikataba yao ipo mwishoni
ni makipa Juma Kaseja wa Simba anayemaliza mkataba Desemba mwaka huu,
Hussein Sharrif wa Mtibwa na Deogratius Munishi wa Azam FC.
Wengine ni beki Shomari Kapombe wa Simba
anayemaliza mkabata Desemba mwaka huu, Pia Amri Kiemba, Juma Nyosso,
Haruna Moshi, Ramadhani Chombo na Abdallah Juma mikataba yao ipo
mwishoni. Kwa upande wa Yanga ni Hamis Kiiza.