VIDEO: P-Funk aongelea Ngwair na madawa. Aichana Clouds FM, aikataza kupiga nyimbo zake

Video: Producer mashughuli nchini P-Funk afunguka kuhusu msanii aliyeaga dunia Albert Mangwea, maarufu kama Ngwair. P-Funk azungumzia sababuanavyodhani zilipelekea marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa. Aichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama dhulma kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya. “Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.”
Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records, P-Funk amesema:
“Niko kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote za Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm, sababu ya A, B, and C. Moja wapo kikubwa ni uonevu wa haki miliki. Nyinyi, ndio number one radio station; ndio mnajipotray hivyo. Kisaikolojia wasanii wote mmewateka. Wote wanaona “bila kupeleka nyimbo yangu Clouds, sitofanikiwa.” Mimi cha kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingie. kwamba bila nyinyi tutaweza. Cha pili mnaingiza hela sana ya wadhamini, lakini hamui-distribute kwa wanaohusika. Ambao wanahusika kupewa hela yake hapewi. Mnaingiza mabilioni lakini hati miliki haichezi. kwanini niendelee kusapoti empire kama hiyo wakati mimi ni chanzo cha Clouds FM kuwepo pale. Na mfumo wa kupeleka nyimbo Clouds nilianzisha mimi hapa. So mimi nitakua wa kwanza kujitoa na kuanzisha mfumo mwingine.”
“Tulikua tunakaa kwenye hiki kibenchi na mangwea na kikonyagi chake and always complaining about who? Clouds FM!”

Angalia Video Hapa:

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. i thnk it's about tym for major changez...2Pac's was right, wen he made tht joint 'Changez', for Tanzanian artist they need to work together n b az one family in tht way there will b nobody who can fck with thm, ths is war, they have to fight together..WTF is Clouds FM!!??

    ReplyDelete
  2. mimi john mwaya kutoka south africa! kifo cha ngweir inasemekana kaji overdose na madawa ya kulevya aina ya cocaine ndipo iliposababisha damu kutembea kwa kasi mwelini na moyo haukuweza kuzuia kasi ya damu hiyo na kustop kwa moyo na kusababisha kifo hicho!inasemekana mapigo ya moyo yalikuwa yakibiga sio kawaida.

    ReplyDelete
  3. WE SUPPORT YOU BRO MAJANII !

    ReplyDelete
  4. safi sana majani leo umenigusa hasa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad