Wadau,
Ninajua kuwa hili kila mtu ameshaliona, kuwa watuhumiwa waliokamatwa
mpaka sasa kuhusiana na mlipuko wa Arusha wamefikia 10 lakini jina
lililotajwa na linaloendelea kutajwa kwa nguvu ni moja kisa ni la
Kikristo? Ni watu wangapi ambao ni wapagani lakini wana majina ya
kikristo? Ni watu wangapi wenye majina bandia kwa sababu wanazozijua
wao? What if jina hilo limetengenezwa? Halafu sitegemei kuona majina
matatu ya mtu mmoja Mwafrika hasa Mtanzania halafu yote yakawa ya
Kikristo (angalau moja lingekuwa la kibantu).
Point yangu hapa ni kuwa ninajua Serikali inafanya hivyo makusudi ili
kuwaondolea watu hisia za kuwa tukio hilo halina uhusiano na udini,
nafikiri wanatumia mbinu ya kitoto sana kwani iko wazi mno! TISS
wanafanya kazi gani wasije na strategy bora kuliko hii?
Ni wazo tu!
Source:JF