Ni muda mrefu sasa kumekuwa na wimbi la watangazaji au maripota wa television na radio wasiomudu kutamka maneno ya kiswahili wanapokuwa wakiripoti/wakitangaza au wakisoma hasa taarifa ya habari.Hii imekuwa kero unapomsikia ripota anatamka maneno mfano bizaa(bidhaa),feza(fedha)saman i(thamani)taalifa(taarifa)n.k. Kifupi matumizi ya r/l,th/s na dh/z ni kero iliyopitiliza kwa hawa watu kwani huondoa ladha ya matamshi ya kiswahili.Sasa swali ninalojiuliza ni vp watu hawa walifaulu usaili(interview)ktk vituo husika na zaidi wanaendelea kuharibu tu.Walifaulu vp mitihani yao tangu shule za msingi mpaka kupata kufikia elimu ya juu? Je maboss hawawasikizi wakawarekebisha? on job trainning hakuna?hata daily briefing pia hakuna?Enyi waandishi nguli mlioko humu jamvini tusaidieni kujadili.
Watangazaji/Maripota Hawa Walipataje Kazi?
4
May 12, 2013
Tags
Kweli yani inakera mno. Wanaongoza clouds na dtv. Jamani jamani umburura mtupu. Hembu anagalieni kina Charles Hillary walivyokua. Du majanga
ReplyDeleteKweli yani inakera mno. Wanaongoza clouds na dtv. Jamani jamani umburura mtupu. Hembu anagalieni kina Charles Hillary walivyokua. Du majanga
ReplyDeleteleo umeongea POINT kwa kweli tatzo ya kaz za kupeana hlf hawajui n rahc sana kwao kufanya watoto washike kitu ambacho c sahihi
ReplyDeleteCheap labour
ReplyDelete