Leo asubuhi katika taarifa ya habari iliyosomwa na kituo cha ITV, wateja wametahadharishwa na wizi ulioshamiri katika Bank mbalimbali na kutakiwa kucheki account zao mara kwa mara.
Nimeguswa kupost hii mada tuweze kuijadili kidogo kutokana na kuwa mimi binafsi nilikuwa natarajia kuandika hii habari kabla ya taarifa ya habari ya leo.
ni kweli kuwa wizi umeshamiri sana hivi karibuni, mi nina shuhuda za ATM zinavyochezewa na pesa za wateja kuchukuliwa kwa njia tofauti tofauti. kuna wateja wanakwenda kudroo fedha wanakuta hawana fedha, wakiingia bank kuuliza, tena hapo waone seriousness yako wanakupiga kiswahili, hasa ukitaka kuonana na meneja wanazirudisha huku wakikuambia nitatizo tu lilijitokeza nenda kachukue zimesharudi. wakati mwingine unaingiza kadi na kupitia process fedha zinajihesabu lakini hazitoki, ukienda bank unakuta mko wengi mliopatwa na hiyo hali, hapo bank wanaahidi kuzirudisha katika siku 3 za kazi. wakikuona wewe sio mkali unaweza kupiga wiki 3 ukifuatilia hiyo pesa.
yanayosemwa mitaani ni kuwa wafanyakazi hasa vijana wapya kazinia ndio wanaocheza zaidi hiyo michezo, aidha ni njia ya kukopa kwa hila na kufanyia miradi yao au ndio unaweza kuibiwa kabisa kwa njia hiyo, hasa ukiwa lege lege. nilikuwa nafatilia hela zangu na wafanyakazi wenzangu niliowashirikisha kila mmoja akaeleza jinsi kwa vipindi tofauti kila mmoja alivyoweza kupata usumbufu wa fedha zilizochukuliwa kwa ujanja. na asilimia kubwa ni wafanyakazi wenyewe, tetesi ni kuwa hata watu wanaochukua fedha nyingi kwa sababu mbalimbali huvamiwa wakitoka nje ya bank kutokana na taarifa zinazotolewa na wafanyakazi wa bank kwa majambazi wanaozagaa nje karibu na banks.
sasa kwa maana hiyo, tunawaomba viongozi wa banks watoe semina kwa hawa vijana wadogo na hata wakubwa wanaojihusisha na wizi huu. kutoka katika maisha sio hivyo, huu ni wizi na ujambazi, wajifunze kuwa wavumilivu na kafanya kazi kwa bidii. kijana anataka akianza kazi katika miezi 6 awe mbali, gari nyumba na anasa , jamani hiyo sio life.
wasiige mafisadi kwa wizi, unaweza ukawa na bidii zako na uaminifu na bado ukafanikiwa ukaishi tu maisha mazuri yasiyo na wasiwasi, vijana uzalendo mnauua kwa tamaa kwa kujilinganisha na wezi, muche kabisa. kuna wale ambao ni waaminifu na wana jitihada zao binafsi, hao tunawasifu sana, na wengine waige hivyo tutaondokana na shaka na kurudishana nyuma kunakoendelea sasa hivi