Timu ya Yanga imeicharaza Simba mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika hivi punde.
Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambao umeingiza zaidi ya mashabiki 60,000. Katika mechi hiyo imevuta mashabiki kutoka Morogoro, Tanga, Arusha, na mikoa mengine mbali ya mashabiki wa Jiji la Dar es Salaam.
Yanga wamepata bao la kwanza kupitia Didier Kavumbagu katika dakika ya 5 baada ya kuunganisha mpira wa kichwa hadi nyavuni.
Wakati Simba wakiongeza presha langoni mwa Yanga katika kipindi cha kwanza, walipata penanti baada ya Cannavaro kumshika Ngassa kumzuia asielekee kuliona goli Yanga.
Kutokana na patashika hiyo muamuzi aliamuru penanti ipigwe kuelekea langoni mwa Yanga, lakini mpigaji alikosa bao baada ya kupiga mpira na kumlenga Batez.
Katika kipindi cha pili, timu zote zilicheza mchezo mkali, kila moja ikiwania kupata goli,na Yanga ilifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 63 lililofungwa na Hamisi Kiiza.
Kutokana ushindi huo Yanga imefikisha pointi 60, Azam pointi 51 na simba pointi 45, Kagera Sugar pointi 41, Mtibwa Sugar 39,Coastal Union 35, Ruvu Shooting 32,JKT Oljoro 29, Prisons 29,
Ruvu Stars 26, JKT Mgambo 25, Polisi Moro 22, Toto Africans 22, na African Lyon 19.
Katika hatua nyingine, vyanzo vyetu vya habari vimebainisha kwamba mechi kati ya Simba na Yanga ambayo imechezwa Leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, TFF wamekusanya zaidi ya Sh330 milioni.