BABY MADAHA AHANGAIKA KUMKIMBIA MWIZI WA CHUPI ZAKE HUKO MIKOCHENI

KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu na muziki Baby Joseph Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa nguo zake za ndani alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni jijini Dar.
Chanzo chetu cha habari ambacho ni shosti wa karibu wa mwanadada huyo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitiririka:
“Alizifua kama dazeni nzima hivi na kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake. Heh! Kumbe vibaka hawaachi kitu, waliruka fensi wakazichukua pamoja na ndala.”
Katika kujua ukweli wa habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Baby Madaha na alipopatikana alisema ni kweli alilizwa nguo hizo na kudai anafanya jitihada za kuhama kwani eneo analoishi limezidi kwa wizi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad