Ugumu wa game la muziki nchini umewafanya wasanii wengi kubuni njia mbadala (za kimafia zaidi) kutengeneza ‘keek’ mjini kama wasemavyo vijana wa siku hizi.
Wengine wamewahi kusambaza picha za uongo kuwa walikamatwa na madawa ya kulevya ili kuitengenezea njia nzuri ngoma mpya,(sikumbuki kama stunt hii ilifanikiwa, I guess it flopped). Wengine huyatumia magazeti kutengeneza stunts za kila aina ilimradi tu majina yao yasitoke midomoni mwa mashabiki wa muziki. Njia hii imewasaidia wengi lakini wengine stunts zao ziki’backfire’ na kuwaletea timbwili la kufa mtu mtaani.
So katika muendelezo huo wa kutafuta keek mjini, rapper Baghdad ameamua kuwa ‘kreative’ kidogo. Vipi kama ukiwasikia maadui wawili kimuziki ambao ni kama Paka na Panya kwenye ngoma yake? Inasound poa sio? Rapper huyo ameamua kucheza mchezo ‘mchafu’ kwa kuwakutanisha Nay wa Mitego na Chidi Benz wenye beef bila wao kujua.
Alichofanya Baghdad ni kuwaambia kila rapper katika muda wake kuwa angependa kumshirikisha. Nay wa Mitego alipewa kazi ya kuipamba chorus ya ngoma hiyo iitwayo ‘Waambie Nipo’. Nay bila kinyongo aliingiza sauti zake na mwisho kuweka outro. Kwenye outro Nay anasikika akisema ‘mngenipa hata verse moja tu niwaharibie humu, mna bahati’
Sikiliza wimbo huo hapa:
Source: Bongo 5