China. Barack Obama na Xi Jinping wamemaliza
mkutano wao wa kwanza kati ya China na Marekani, wakiweka hali ya
kuelewana na kukubaliana kuhusu sera na kupata jawabu kuhusu Korea ya
Kaskazini, hali ya hewa na mtandani.
Marais hao walitumia saa nane pamoja katika muda
wa siku mbili, katika makundi ya yaliyokuwa na ukaribu ya wafanyakazi,
katika chakula cha jioni, pamoja na kutembea katika bustani nzuri katika
eneo lililotunzwa vizuri katika Jangwa la Califonia.
Ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya China na
Marekani tangu Xi mwenye umri wa miaka 59 kuchukua madaraka kamili ya
nchi hiyo Machi na Obama mbunifu wa kupanga upya diplomasia ya Marekani
kuelekea Bara la Asia ambaye anatazamwa kwa jicho la shaka na China,
kuchukua madaraka katika kipindi cha pili cha utawala wake.
Pande zote mbili zilitaka kulegeza mazungumzo hayo
kati ya China na Marekani kuwa ya kawaida, na hali hiyo imeonekana
kufanikiwa.
Katika wakati fulani Obama na Xi, wakitafuta
msimamo wa pamoja kama wanasiasa, walitayarisha mitazamo yao katika
kuelekeza kule ambako wanataka kuyaelekeza mataifa yao.
Wakati Xi alipoondoka maofisa wa Marekani walisema
, viongozi hao wawili walizungumza moja kwa moja kuhusu maeneo ya
matatizo, usalama katika mtandao, wakashutumu kukwama kuhusu mpango wa
kinyuklia wa Korea ya kaskazini na kukubaliana kuhusu msukumo mpya wa
pamoja kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.