"HIVI NDIVYO NILIVYOAMBUKIZWA UKIMWI NA GIRLFRIEND WANGU NILIYEMPENDA KWA DHATI "....MUATHIRIKA

Hili suala ni gumu kuliko linavyofikirika na jamii na watu ambao hawajapatwa na mikasa migumu. Ndio maana unyanyapaa unaendelea kutawala sana humu nchini na tatizo linazidi kushamiri. Nilikuwa na mchumba ambaye nilimpenda sana na ndiye niliyemuweka kuwa chaguo langu la maisha.

Mwanzoni mwa uhusiano wetu tulikuwa tukifanya mapenzi kwa kutumia condom na baadaye tulikuja kuacha kutumia baada ya kupima several times na kuona tupo vizuri na tulikuwa tumeshakubaliana kuja kuishi pamoja. Nilimtambulisha kwa ndugu zangu kama ndiye ndugu yao atakayeongezeka na yeye alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake.
Miaka ilivyozidi kwenda niliona mabadiliko kwa mwenzangu kitabia kwani kuna wakati alikuwa akinidanganya kwamba amesafiri kumbe yupo na hajaondoka. Kumbe mwenzangu alishaanzisha uhusiano na wazee wa mujini wenye pesa zao hivyo akawa ananipotezea kwani kwa wakati huo ndo nilikuwa namalizia mwaka wangu wa mwisho chuoni.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani ilifika kipindi akanambia ile mipango tuisitishe. nilipomuuliza kwa nini, hakuwa na jibu la wazi. Ilinichanganya sana lakini nilipata faraja kutoka kwa rafiki zangu na ndugu nikatulia. Baada ya miezi kama sita kupita niliamua kwenda kupima na nikagundulika kwamba niko na maambukizi ya VVU, nilichanganyikiwa sana na niliona kama hakuna haja ya kuishi tena.

Sikumwambia mtu mwingine zaidi ya doctor mmoja na mimi mwenyewe kuugulia maumivu yangu peke yangu ila kuna wakati ndugu na jamaa walikuwa wakiniona nimebadirika ila nawaambia hakuna shida yoyote na nipo kawaida. Nilijitahidi kutokukaa peke yangu kwani mawazo ndo yangenizidia.

Mpaka sasa hivi nipo vizuri na nna afya njema ila napata wakati mgumu sana kwani wasichana wengi wanaonesha dalili za kutaka kuwa na uhusiano na mimi lakini nawaonea huruma sana kwani inaniuma sana nikifikiria kumwambukiza mtu mwingine. Wengi wao nimekuwa nikiwakwepa mpaka wengine wananitangazia kwamba jogoo wangu hawiki, huwa inaniuma sana kwani sitaki wajue na sipendi kuwafanya wawe kama mimi.


 Nisiwasumbue sana, naomba nihitimishe kwa kusema; hili tatizo ni gumu sana hasa unapokuwa wewe ndiwe 100%. Tupigeni vita unyanyapaa ili watu wasiwe na mawazo ya kwamba TUFE WENGI. Pia unayemnyanyapaa hujui aliupata vipi kwani si kila mwenye VVU alikuwa kuruka njia. Kuna wengine wameupata kutoka kwa watu wanaowaamini sana! Na wengine miaka ya leo wamezaliwa nao hivyo sio kosa lao kwa hapo walipo.

Source:Talk Bongo Blog

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmnh....very sad story.Wasichana wengi siku hizi wana tamaa na vitu vya anasa kama magari,nyumba nzuri n.k hivyo huwapelekea kupata magonjwa yasiyo na tiba.Pole ndugu

    ReplyDelete
  2. pole sana kaka mungu aendelee kukupa uvumilivu pia jiunge na mashirika yakupambana na maambukizi dhidi ya ukimwi

    ReplyDelete
  3. tukipata watanzania wenye moyo kama wa huyu jamaa hakika tutapiga hatua kwenye nyanja mbalimbali za kimaisha,MUNGU akusafishie njia katika harakati yako,im inspired

    ReplyDelete
  4. Pole kaka, na mimi nina kesi kama ya kweko,mimi ni msicha wa umri wa miaka 26 nilikuwa na boyfrend wangu niliyempenda wakati tukiwa kwenye tendo mwenzangu alikuwa anavua kinga pasipo mimi kujua, siku moja walikuja watu kupima ukimwi mtaani kwetu kuna uwanja waliweka mahema pale, wakawa wanatangaza pima ushinde, sabuni dawa ya mswaki, mafuta na vitu vingine. kwa kujiamini nikasema ngoja nikajishindie chochote kati ya vile kwani najiamini sina huo ugonjwa, matokeo yalipotoka nikaambiwa nimeathirika , kwakweli nilichanganyikiwa sikuamini kabisa, nikaambiwa nirudi tena kesho yake kwa ajili ya kurudia, matekeo yakawa ni yaleyale, kwakweli nilikuwa katika wakati mgumu sana, nilikuwa nasoma chuo flan, naishi na mjomba wangu kwani sina wazazi na ninadigi zangu watatu mimi ndio wakwanza nilitamani nife tu niwafate wazazi wangu kuliko hali ile niliyokuwa nayo, siku moja nikamshirikisha rafiki yangu mmoja tu hata yule kaka sikumwambia mpaka leo hii naandika ujumbe huu , na hata akiniita huwa namkwepa na hata akinipigia sipokei mpaka anataka kunifanyia fujo. kwani najua alinifanyia makusudi kwakuwa alijua nampenda kwakweli inauma sana sana sana sana. Sijuia hatma ya maisha yangu ndoto ya kuolewa na kupata watoto imepotea kabisa, huwa naenda clinic kila Jtatu ya mwisho wa wiki ya kufungia mwezi nashuku tangu nipime ni miaka miwili sasa na sinywi dawa zaidi ya vidonge vya kuzuia homa tu, kwa sasa nina afya njema tena kushinda hata kabla sijapima. JAMANI HEBU TUWE NA HOFU YA MUNGU JAMANI TUSIWAAMBUKIZE WENZETU TUNAOWAPENDA TENA AMBAO HAWANA HATIA , kwa sasa kuna kijana ananipenda sana na anaifuatilia sana lakini siko tayari kuuwa bila hatia, huwa najiskia kufanya mapenzi lakini nikikumbuka yaliyonikuwa basi nyege zote huniisha. TUBADILIKE JAMANI.

    ReplyDelete
  5. Ajali kazini kaka uguwa pole umetupa upande wako wa hadithi upande wa mwenzio hatuja usikia vipi tutamini kwa ni yeyey aliyekubandika hayo marazi ?

    ReplyDelete
  6. Ningependa kukushauri na kukupa Moyo
    Kapata ukimwi sio mwisho wa maisha
    Nimepata ukimwi mwaka 2003 na nina mume
    Nilikuja kama ni VVU mimba ilivyotoka kupimwa
    Nikaambiwa Nina VVU but mme wangu Hana
    Nililia sana ndiyo nikajua ndiyo mwisho wa maisha yangu, but mume wangu anemia support kubwa sana
    Na mpaka Leo Nina mtoto Ana miaka 7 na Hana VVU
    Na najiona Mimi ni mzima kushinda Mtu mwingi, sometimes nasahau Kama Nina VVU na virus zangu ni undercount able. Ni 10 years sasa tangu nimejua,Naamini kipata ukimwi sio Umalaya tena inaweza kumtokea kwa Mtu yeyote, Mungu yupo pamoja nasi . Utashangaa wewe una ukimwi Ufi wazima wanakufa. I am happy to share with you today kwa sababu Nina nguvu na Afya nzuri na nafanya kazi na hakuna anayejua Nina VVU.Please never give up ukijua
    Una ukimwi ndiyo life yako imeisha it just started na kubadilisha maisha yako uishi vipi.Ukimwi ni sawa na malaria tu kwani si Luna watu wanakufa kwa malaria.
    Ebu fikiria Mtu mwenye cancer anapoambiwa siku zake za Kuishi zimebaki chache !!!!!!?
    Mungu awabariki sana

    ReplyDelete
  7. Hii ndiyo dunia tulimo ndugu yetu. Pole sana kwa mkasa huo. Mtumainie Mungu naye atakushindia..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad