MWANAMITINDO daraja la kwanza Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika
mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya
wapendanao.
Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi
ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa
Instagram.
“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa
jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike
alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.
Baada ya
kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake
na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana
akazisevu katika simu yake.
Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza.
Baada ya paparazi wetu kuzitia kibindoni picha hizo, alimsaka Jokate kwa njia ya simu ili azitolee ufafanuzi.
Mwandishi: Haloo Jokate…
Jokate: Nitumie meseji nipo kwenye kikao.
Mwandishi
wetu alimtumia meseji kama alivyoshauri staa huyo ambapo alimtaka
amtambulishe mwanaume huyo na aeleze kama ndiye mpenzi wake mpya,
hakujibu chochote.
Paparazi wetu alimtumia meseji ya pili kumsisitiza atoe majibu ndipo alipojibu kwa kifupi:“Hapana mumy!”
Pamoja
na majibu hayo, paparazi wetu alimtumia meseji nyingine kumuuliza kama
siyo mpenzi wake ni nani lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakujibu
chochote.
Kabla ya kumuanika mwanaume huyo, Jokate aliwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku pia akitajwa kutoka
na mcheza kikapu, Hasheem Thabeet.
Source:Global Publisher
Acheni kupindisha maneno... Instagram aliandika kabisa ni fan wake... Khaaaa mkikosa cha kuandikaga jamani muache
ReplyDelete