KIPA wa Simba, Juma Kaseja, amesema kwa sasa hawezi kujiunga mapema
katika mazoezi ya kikosi hicho kutokana na kwamba hana mkataba na klabu
yoyote.
Kauli hiyo ya Kaseja inakuja kufuatia kipa huyo mkongwe
kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, ambao ulifikia tamati
mwishoni mwa msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Jumatano,
Kaseja alisema kwa sasa hawezi kujiunga mapema na kikosi hicho
alichokitumikia hadi msimu uliopita kwa kuwa hana mkataba na timu hiyo
baada ya ule wa awali kumalizika.
Kaseja alisema kwa sasa atakuwa na
mapumziko ya siku chache baada ya kumaliza majukumu ya Taifa Stars,
ambapo atajua hatima ya timu atakayoichezea msimu ujao ndani ya siku
saba kuanzia juzi.
“Ukiniuliza nitajiunga lini katika mazoezi ya
Simba, sidhani kama nitakupa jibu zaidi ya sijui, kutokana na sasa sina
mkataba wowote na Simba, mimi sasa ni mchezaji huru, mkataba wangu na
Simba ulishakwisha,” alisema Kaseja huku akiongeza kwa kusema:
“Hivi
ninavyoongea na wewe (juzi jioni), ndiyo kwanza hata nyumbani kwangu
sijafika, natoka katika kambi ya timu ya taifa, nataka kwanza
nikapumzike kwa siku kadhaa na baada ya hapo nadhani ndani ya siku saba
nitajua nini nifanye na wapi nitasaini.”
Mpira ushamkataa...hana jipya
ReplyDelete