Hiyo inatokana na uamuzi unaotajwa kufikiwa na
majaji wa ICC ambao wametoa mapendekezo wakimtaka Rais wa ICC aangalie
umuhimu na kutoa ruhusa ya kesi hiyo kusikiliziwa nchini Kenya au kama
ikishindikana basi isikiliziwe nchini Tanzania.
Uamuzi huo unaweza pia kusababisha athari za
kuichochea mahakama hiyo kuhamisha pia kesi ya aina hiyo inayomhusu Rais
Uhuru Kenyatta ambaye pia mawakili wake wameomba kesi dhidi yake
ihamishiwe nchini Kenya au Tanzania.
Ruto pamoja na mtuhumiwa mwenzake, aliyekuwa
mtangazaji wa Redio, Joshua Arap Sang wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ya
uhalifu dhidi ya ubinadamu wakidaiwa kuhusika kuchochea vurugu za baada
ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu
1,000.
Mapendekezo hayo yametokana na ombi hilo
lililotumwa Januari 24 mwaka huu ambalo lilikuwa bado likiendelea
kujadiliwa n amamlaka zinazohusika kwenye mahakama hiyo.
Februari mwaka huu, Mwendesha mashtaka mkuu wa
ICC, Fatou Bensouda aliieleza mahakama hiyo kwamba hana pingamizi iwapo
itakubalika kesi hiyo isikiliziwe Tanzania au Kenya.
Hata hivyo mahakama hiyo ilieleza kuwa mapendekezo
hayo bado yanaendelea kujadiliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na
mahakama hiyo.
Hata hivyo, jana ICC ilitoa taarifa ikisema kesi
dhidi ya Ruto anayetuhumiwa kufanya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu
itaanza Septemba 10 mwaka huu.
Taarifa hiyo imesema majaji wameamua kupanga tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo mapema zaidi kuliko ilivyopangwa awali.
Rais Kenyatta na naibu wake wanahitajika
kupandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka yanayowakabili ya uhalifu
dhidi ya ubinadamu, makosa ambayo waliyafanya wakati wa vurugu
zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Rais wa mwaka 2007/08.
- Kumpandisha cheo Kamuhanda ni kuwakebehi Watanzania
- Vyama vyetu vinapogombea itikadi za kuazima Ulaya
- Kugombea urais ni kikohozi, kuficha huwezi
- Katiba Mpya; Zanzibar kwanza, siasa baadaye
- Mulugo azungumzia uchache wa walimu nchini
- Kesi dhidi ya Ruto kuhamishiwa Kenya au Tanzania
- Spika ampandishia Mbatia kwa kutamka ‘ sumu’
- Azam yawatupia virago Babi, Uhuru
- TFF yahofia usalama Simba, Yanga
- Ngwair kuagwa leo
- Tanzania mpya
- Rais apunguziwa uwezo
- Viti Maalumu kufutwa, ubunge kuwa na ukomo
- Muungano ni Serikali tatu
- Hoteli ya ‘kigogo’ yapigwa mnada Moshi
- Kibanda : Sitanyamaza kwa unyama huu
- Undani kifo cha Ngwea
- Katiba Tanzania Bara yanukia
- WanaCCM Zanzibar wamshukia Maalim
- Nec yapendekezwa kuvunjwa, iundwe tume huru
WOW just what I was looking for. Came here by searching for Gerardus Mercator
ReplyDeleteAlso visit my homepage :: Time Warner Cable installation