KIJIJI CHA NGONO CHAFICHULIWA HUKO SINZA,MAKAHABA WAAHIDI KUTOACHA KAZI HIYO


NI hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani
Kwa mujibu wa takwimu za kiserikali, eneo hilo
(kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori) limekubuhu kwa wasichana kujiuza nyakati za usiku huku makao yao makuu yakiwa eneo la Afrika Sana hasa pembezoni mwa Corner Bar.

Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa ya eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe , alisema:
 “Tumejitahidi sana kushirikiana na polisi ili kutokomeza ukahaba eneo hilo lakini wapi! Hawa mabinti ni wabishi, mbaya zaidi wamelifanya eneo hili kuwa la ngono.
“Watoto wetu wanapita usiku pale wanawaona wanavyofanya, wanatuharibia kizazi kijacho, kama wao wamejishindwa wasiwaambukize wengine.”
Siku ya tukio, saa tisa usiku,  askari wa ulinzi shirikishi walijipanga kwa ajili ya kuufumua mtaa huo huku wakiwa na tahadhari kufuatia habari za kiintelijensia kudai kuwa, makahaba hao walipanga kuua mtu punde watakapovamiwa.

Askari hao wakiwa kwenye doria ya kila usiku, waliwavamia makahaba hao eneo lenye majani madogo katikati ya Afrika Sana na Mapambano upande wa yadi ya Mwanamboka wakiwa na wateja wao wakifanya ngono hadharani.
Katika hali iliyoonesha makahaba wamejiimarisha kwa ulinzi siku hizi, wakati wa zoezi hilo, machangu hao sanjari na vibaka  wanaowaunga mkono wakisemekana ni ‘walinzi’ wao, waliokota mawe na kuwarushia askari hao hali iliyozua tafrani zaidi.
Ndipo piga nikupige ilipozuka ambapo askari walionesha umahiri wao wa kupambana na wahalifu kwa kuwadhibiti kwa vichapo vya hapa na pale na kufanikiwa kuwaweka wengi chini ya ulinzi.
Kuona hivyo, baadhi ya makahaba na wateja wao walifanikiwa kuwachoropoka askari bila nguo na kutokomea gizani hivyo kulifanya eneo hilo kuwa jeupe.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya makahaba waliokimbia walijikuta wakiacha kwenye majani nguo zao za ndani na kuzua maswali kwamba ni kwa nini hawakuwa wamezivaa!


“Jamani hizi si nguo zao za ndani? Ina maana wakiwa kazini hawavai siyo? Wanakuwa tayaritayari kwa kazi? Jamani!” alisema kwa mshangao mkubwa mmoja wa askari hao.

Licha ya kuwa chini ya ulinzi mkali, baadhi ya makahaba walionaswa walikuwa wakiwalalamikia askari hao kwamba wanawafuatafuata wakati kila mtu siku hizi anaangalia atakulaje!

“Mnatuonea bure, nyie mnakula kivyenu na sisi mngetuacha tule kivyetu, hao watoto wenu mnaosema tunawaharibu usiku huu wao wanatokea wapi na wanakwenda wapi?” alisikika akisema kahaba mmoja aliyekuwa mtata kuwekwa chini ya ulinzi.


Mwingine akadakia: "Kama mnataka tuwape uroda si mseme, mnatukamata kila siku kwani tunawatibulia nini majumbani mwenu? Lini tumekuja kuwaghasi wakati mmelala na wake zenu?”

Uchunguzi wa kawaida ulibaini kuwa muda rasmi wa
makahaba hao kuwasili eneo la Corner Bar ili kuanza ‘kazi’ ni saa mbili usiku japokuwa wapo wanaoripoti mapema na kufanya biashara hiyo kwa wizi kulingana na wateja wenye ‘kiu’ nyakati hizo.

Licha ya kuwa chini ya ulinzi, makahaba hao waliahidi endapo watapelekwa polisi na kutoka watarejea eneo hilo kujiuza kwani ndiyo ajira inayowafanya waendelee kuishi katika Jiji la Dar es Salaam, kusomesha watoto vijijini kwao na kuwasaidia wazazi wao mahitaji mbalimbali.

“Hata kama mtatupeleka polisi, tutarudi tu hapa, sisi tunasomesha watoto, tunasaidia wazazi wetu vijijini, pia tunaishi Dar kwa sababu ya kipato hiki cha kuuza miili yetu, acheni hizo,” mmoja wa makahaba hao alisema bila kumung’unya maneno.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad