“Nikilala naota, naota kama unaniita, ila nafsi inasiita mpenzi ipo siku ntaitika…..” ni mashahiri ya wimbo mtamu na uliobeba hisia nyingi “Zamani”, ambapo Aboubakary Shabani Katwila a.k.a Q Chief alimshirikisha ‘Binti machozi’ (wa wakati ule). Baada ya miaka kupita Q Chilla na Lady JayDee ‘Anaconda’ wamerudi tena studio kutengeneza ‘hit’ nyingine ‘SUKARI’.
Jumatano (June 26) Lady JayDee alitweet picha yake na msanii Q Chilla wakiwa pamoja na mshindi wa tuzo ya producer bora wa mwaka KTMA (2013) Man Water katika studio ya Combination Sound wakipika hit song yao mpya.
Jide alitweet “Mtu 3 ndani ya studio. Mwaikumbuka Zamani – Q Chief feat Jide?? Nikilala naotaa, naota km unaniita. Sasa yaja mpya”.
Baadhi ya watu waliuliza kama hii ni remix ya wimbo waliowahi kufanya “Zamani” lakini Jide alijibu kuwa huo ni wimbo mpya unaoitwa SUKARI…“Sukari – Qchillah & Jide another hit ??? ☺ #Justasking”, alitweet Jide.
Hiki ni kipindi ambacho Lady Jay Dee anafanya vizuri na album yake mpya ‘Nothing But The Truth’. ‘Joto Hasira’ pamoja na ‘Yahaya’ ni nyimbo mpya za Jide ambazo kama hutazisikia Radio C basi utakutana nazo Radio E au ikikupita Radio A utaisikia Radio T na ukizikosa kote huko utapishana nazo katika bajaji/boda boda au sehemu za starehe, kwa lugha nyingine ni hit songs.
Hivyo mimi binafsi naamini huu utakuwa ni muendelezo wa mafanikio hayo kwa Lady Jay Dee ambaye (June 14) alisheherekea miaka 13 katika muziki, lakini pia inaweza kuwa njia nzuri ya kumrudisha Chilla ambaye anaonekana kutofanya vizuri sana kwa sasa.