MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga
Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss
Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo
lilipokuwa likiendelea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita
katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo
huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji la mkoa huo.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na
kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi
ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima
ya Miss Tanzania.
Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na
kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu
wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.
Mbali na
Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel
(20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu,
inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.
Lundenga
alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kamati yake inataka kuendeleza
nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.
Uyo mnafki...atakua kanyimwa yale mambo yetu ndomana anamtafutia sababu
ReplyDeleteumiss ni upumbavu 2 na wanaoenda kuangalia na kushughulika
ReplyDelete