Washington- Rais Obama atapokwenda Afrika Kusini mwa Sahara mwezi huu, taasisi zenye jukumu la usalama wake hazifanyi lelemama.
Mamia
wa mashushushu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais wa Marekani (US Secret
Service) watasambazwa katika maeneo ya usalama huko Senegal, Afrika ya
Kusini na Tanzania. Manowari ya Jeshi la Vita la Marekani inayotumika
kubeba ndege za kivita au nyambizi, ikiwa na matabibu waliokamilika,
itakuwa imeegeshwa pwani kwa ajili ya dharura.
Ndege
za kijeshi za kubeba mizigo zitasafirisha magari 56, ikiwa ni pamoja na
'limousines' 14 na magari ya mizigo matatu yote yakiwa na makasaha ya
vioo visivyopenya risasi vitakavyowekwa katika madirisha ya hoteli
atakazofikia Obama na familia yake. Ndege za kivita zitakuwa
'zikizurura' angani kwa zamu, kuwezesha ulinzi wa masaa 24 katika 'anga
ya Rais' ili ziweze kuchukua hatua pindi ndege ya adui itakapoingilia
kati.
Maandalizi
haya mhsusi ya kiusalama-ambayo yataigharimu Serikali ya Marekani
makumi ya mailioni ya dola- yapo kwenye nyaraka ya siri iliyopatikana
kwa gazeti hili (la Washington Post). Wakati maandalizi hayo yanaendana
na mengineyo katika safari nyingine, nyaraka husika inatoa picha ya
jitihada za hali ya juu katika kumlinda Amiri Jeshi Mkuu wa wa majeshi
ya Marekani anapokuwa ziarani nje ya nchi hiyo.
Safari
yoyote ya Rais, kama za wiki hii huko Ireland ya Kaskazini na Ujerumani,
ni zina changamoto na gaharama kubwa kilojistiki.Lakini safari hii ya
Afrika inakuwa ngumu zaidi kutokana na sababu mbalimbali, na inaweza
kuwa yenye gharama zaidi kuliko zote katika utawala wa Obama, kwa mujibu
wa watu walio karibu na maandalizi hayo.
Familia
ya Obama inatarajiwa kutembelea nchi hizo tatu kuanzia June 26 hadi
Julai 3 ambapo maafisa wa Marekani ndio watakaokuwa na jukumu la
kuhudumia takriban kila kitu, badala ya kutegemea hudma za polisi, jeshi
na hospitali katika nchi wenyeji.
Rais
Obama na mkewe pia WALIPANGA KUFANYA ZIARA KWENYE MBUGA ZA WANYAMA
('SAFARI' kwa Kiingereza), ambayo ingehitaji kikosi cha kupambana na
mashambulizi dhidi ya Rais kubeba silaha maalum zenye risasi maalum za
kumudu kuwaangamiza duma, simba na wanyama wengine hatariu wa mwituni
endapo wangekuwa tishio, kwa mujibu wa nyaraka hiyo
Lakini
maafisa walisema Alhamisi kuwa ZIARA HIYO (YA MBUGANI) IMEAHIRISHWA [ NA
HII NDIO SABABU ILIYOPELEKEA UZUSHI WA BAADHI YA MABLOGA KUWA ZIARA YA
OBAMA KUJA TANZANIA IMEFUTWA] na badala yake imeandaliwa ziara ya
kutembelea Kisiwa cha Robben pembezoni mwa pwani ya Cape Town, Afrika
Kusini, ambapo Nelson Mandela alifungwa kama mfungwa wa kisiasa.
Gazeti
hili lilipowauliza maafisa wa Ikulu ya Marekani (White House) kuhusu
ZIARA YA MBUGANI ('safari') mapema mwezi huu,walisema hawajafikia uamuzi
wa mwisho kuhusu suala hilo.Afisa mmoja wa Ikulu hiyo alieleza Alhamisi
kuwa kufutwa kwa ziara hiyo ya mbugani hakukuhusiana na udadisi
uliofanywa na gazeti hili hapo awali.
"Hatuna
nyenzo zisizo na ukomo kufanikisha safari ya Rais, na tumeipa
kipaumbele ziara ya Kisiwa cha Robben badala ya ziara ya MASAA MAWILI
mbugani nchini Tanzania," alieleza msemaji Josh Earnest. "Kwa bahati
mbaya, hatuwezi kufanya mambo yote mawili." [HEBU ANGALIA HAPA JINSI BLOGA HUSIKA ALIVYOCHAPIA SENTENSI HIYO NA HATA JINA LA MSEMAJI HUYO WA IKULU]
Nyaraka
za ndani za kiutawala zilizosambazwa mwezi April zilionyesha kuwa
familia ya Obama ilipanga kufanya ziarazote mbili- ya mbugani na
kisiwani, kwa mujibu wa mtu anayefahamu maandalizi hayo.
Marais
wa zamani, Bill Clinton na George W. Bush pia waliwahi kufanya ziara za
mataifa mbalimbali ya Afrika, ambazo zilihitaji maandalizi magumu kama
haya. Bush alikwenda mwaka 2003 na 2008, akiambatana na mkewe katika
safari zote hizo. Mabinti wawili wa Bush pia walisafiri naye katika
ziara ya kwanza, ambayo ilijumuisha 'safari' kwenye hifadhi ya wanyama
katika mpaka wa Botswana na Afrika Kusini.
"Hata
katika nchi zilizoendela za Ulaya ya Magharibi, kiwango cha huduma
kinachohitajika kwa ajili ya ziara ya rais ni cha hali ya juu," alisema
Steve Atkiss, ambaye alikuwa mwandaaji wa ziara akiwa msaidizi maalum wa
hudma kwa Bush. "Kadri unavykwenda mbali zaidi, katika maendeo yenye
maendeleo duni, kwa hakika ni changamoto ya kilojistiki."
Ikulu
ya Marekani na Mashushushu wa Secret Service wamekataa kuzungumzia
mipango ya kiusalama, na wasiaidizi wa kiutawala wametahadharisha kuwa
maandalizi ya safari ya rais hayajahitimishwa.
Safari
za nje za Obama zinakuja wakati taasisi za serikali, ikiwa pamoja na
Secret Service, zinapambana na kukata matumizi kwa lazima. Walizni hao
wa Rais walilazimika kukata dola milioni 84 katika bajeti yao ya mwaka
huu, na mwaka huu Idara hiyo ilifuta ziara za wageni kutembelea Ikulu ya
Marekani (kiutalii) ili kuokoa dola 74,000 kwa wiki ambazo ni gharama
za watumishi kufanya kazi nje ya muda (overtime).
Taarifa
nyingi kuhusu ziara za Rais nje ya nchi hufanywa siri kwa sababu za
kiusalama wa taifa, na kuna ufahamu kidogo tu kwa umma kuhusu gharama
za jumla. Ripoti kutoka Ofisi ya Uwajibikaji wa Serikali ilionyesha kuwa
ziara ya Clinton barani Afrika mwaka 1998 alipozuru nchi sita
iliigharimu Serikali ya Marekani angalau dola miloni 42.7.Kiwango hicho
kilitumika zaidi na Jeshi, ambalo lilifanya safari 98 kusafirisha
watendaji na magari,na kuandaa maendeo ya dharura za kimatibu katika
nchi tano.
Kiwango hicho hakikujumuisha gharama za Secret Service ambazo zinachukuliwa kama siri.
Ziara
ya Obama inaweza kugharimu kati ya dola milioni 60 hadi milioni 100 kwa
kuzingatia gharama za safari za nyuma barani Afrika. Nyaraka ya Secret
Service kuhusu ziara hiyo,ambayo ilionwa na gazeti hii, iliyowasilishwa
na mtu anayeguswa na gharama za ziara hiyo, haikuonyesha Idara hiyo
itatumia kiasi gani cha fedha.
"Miundombinu
inayoambatana na ziara za Rais zipo nje ya uwezo wetu," alisema Ben
Rhodes, Naibu Mshauri wa Usalama wa taifa wa Obama katika mawasiliano ya
kimkakati. "Mahitaji ya kiusalama hayapangiw na Ikulu, hupangwa na
Secret Service."
Maafisa
wa zamani na wa sasa wa usalama wa serikali waliohusika na ziara za
rais walibainisha kuwa watendaji wa Ikulu nao husaidia katika kuainisha
mahitaji hayo, kwani hupanga sehemu za kutembelea na mipaka yake. Secret
Service na Jeshi hufuatilia maandalizi hayo ya ziara yaliyowasilishwa
kwao kwa kutaja mahitaji ya kiusalama.
Maafisa
wa Ikulu ya Marekani wamesema kuwa dhamira ya ziara hiyo imekuwepo
kitambo sasa, na itakuwa ya kwanza kwa Obama kama Rais kutembelea Afrika
Kusini mwa Sahara licha ya 'kusimama' kwa masaa 22 nhini Ghana kwa msaa
22. Demokrasia changa zilizomo kwenye ratiba ya ziara hiyo ni washirika
muhimu wa kiusalama katika eneo hilo, Rhodes alisema.
Obama
atafanya mikutano na kila kiongozi wa nchi atakayotembela kwa minajili
ya kujenga ushirikiano bora wa kiuchumi katika wakati huu ambapo China
inawekeza vya kutosha barani Afrika. Pia atapigia mstari programu za
afya, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Mke wa
Rais, ambaye alitembelea Afrika Kusini na Botswana bila ya mumewe mwaka
2011, atashiriki kwenye baadhi ya amtukio katika ziara hiyo. Hilo pia ni
changamoto la kilojistiki kwa vile naye atahitaji maandalizi tofauti ya
kiusalama kuhusu walinzi na magari, kwa mujibu wa nyaraka hiyo.
Msemaji
wa Secret Service, Ed Donovan, alikataa kuzungumzia maandalizi ya ziara
hiyo. "Siku zote huwa tunatoa kiwango stahili cha ulinzi kutengeneza
mazingira salama," alisema.
Kwa mujibu wa nyaraka ya Secret Service, Obama atakaa siku moja Dakar,
Senegal, siku mbili Johannesburg,Afrika Kusini, na siku moja Dar es
Salaam, Tanzania.
KATI
YA MAGARI 56 KWA AJILI YA ZIARA HIYO NI 'LIMOUSINES' KWA AJILI YA RAIA
NA MKEWE , GARI MAALUM LA MAWASILIANO YA SIMU NA VIDEO, GARI LA KUZUWIA
MAWASILANO YA RADIO KUZUNGUKA GARI LA RAIS, GARI LILILOJITOSHELEZA LA WA
WAGONJWA (ambulance) AMBALO LINAMUDU MAABUKIZI YA KIBAIOLOJIA NA
KIKEMIKALI NA GARI LA VIFAA VYA MIONZI YA X-RAY
Mashushushu
wa Secret Service husafirisha magari kama hayo, pamoja na vioo vya
kuzuwia risasi, katika ziara nyingi, ikiwa ni pamoja na zile za ndani ya
Marekani, msemaji wa Ikulu alieleza. Lakini kwa vile kuna nchi tatu
zinazohusika katika ziara hiyo, kunahitajika seti tatu za maandalizi
hayo,kwa sababu hakuna muda wa kutosha wa kuhamisha vifaa, kwa mujibu wa
nyaraka hiyo.
Mashushushu
100 wanahitajika kama 'waangalizi' - kumudu maeneo ya kumzunguka Rais-
katika kila mji atakaozuru. 66 wanahitajika kumpokea Obama jijini Dar es
Salaam. Kabla 'safari' ya Mbuga ya Taifa ya Mikumi haijaahirishwa wiki
iliyopita, ziada ya mashushushu 35 ilijumuishwa kwenye maandalizi hayo
ili kumlinda Rais, mkewe na mabinti zao wawili, kwa mujibu wa nyaraka
hiyo.
Kadhalika,
kati ya mashushushu 80 hadi 100 watasafiri na kufanya kazi kwa shifti
kwa masaa 24, kwa ajili ya ulinzi wa Obama na familia yake, vikosi vya
kupambana na mashambulizi (counterassault teams) na waandaaji wa
lojistiki.
Nyaraka
hiyo ya maandalizi ya ziara haionyeshi idadi ya mashushushu
watakaohusika na ziara hiyo, japo baadhi watafanya kazi katika kituo
zaidi ya kimoja.
Maafisa
walisema Secret Service haitaki ziara ya Rais pasipo kituo cha hali ya
juu cha jirani cha kukabili maradhi. Kitengo cha utabibu cha Ikulu
hufanya maamuzi kuhusu hospitali gani Rais awapo ziarani nje ya nchi
kinakidhi viwango, kwa kufanya ziara kwenye nchi husika, maafisa
walieleza.
Katika
nchi zinazoendelea, Jeshi la Majini la Marekani huweka 'hospitali
inayoelea' kwenye manowari ya kubeba ndege au nyambizi, jirani.
"Hivi
ndivyo inavyohitajika kuilinda taasisi ya urais wa Marekani," alisema
Atkiss kuhusu mahitaji husika, "pasi kujali nani ni rais."
NIMEITAFSIRI HABARI HII KAMA ILIVYO KATIKA GAZETI LA WASHINGTON POST
Kudadadeki! vp Kikwete anapokwenda kwao?
ReplyDeleteCCM mtatoka tu hamkuzaliwa kutunyanyasa
ReplyDeletemh kweli manjaga
ReplyDeleteDah unbelivable
ReplyDelete