Nchi ya Malawi
imepinga na kulalamika kuhusiana na kusudio la Tanzania kupeleka meli
mbili za abiria katika ziwa Nyasa na kudai, kitendo cha kufanya hivyo
kitaadhiri na kutishia mazungumuzo yanayotafuta suruhisho la muda mrefu
ili kulimaliza mzozo wa ziwa Nyasa (malawi) uliodumu kwa muda mrefu.
Waziri wa Mambo
ya Nje wa Malawi, Efraimu Chiume alikaririwa jumamosi akisema, kwamba
viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania walisikika hadharani wakisema
kwamba serikali ina mpango wa kununua meli sita na mbili zitapelekwa
ziwa Malawi kusaidia kuondoa tatizo la usafiri.
Waziri Chiume
alidai mpango wa kupeleka meli ziwa Nyasa (malawi) umekuja katika hali
ambayo siyo mwafaka ikichukuliwa kuwa mazungumzo yalikuwa yanaendelea
bila matatizo.
Maofisa wa serikali ya Tanzania hawakuweza kupatikana kuliongelea swala hili.
Malawi ambayo iko
upande wa magharibi mwa ziwa inadai kumiliki nusu yote ya upande wa
kasikazini mwa ziwa na huku Tanzania ambayo iko upande wa mashariki nayo
ikidai kumiliki nusu ya upande wa kaskazini ya ziwa wakati nusu ya
kusini mwa ziwa ikimilikiwa na Malawi na Msumbiji kwa pamoja.
Mwezi uliopita
malawi ilirudi kwenye mazungumzo ambayo mwanzo ilijitoa baada ya
kuilalamikia Tanzania kwa kuwatisha wavuvi wa Malawi, madai ambayo
Tanzania iliyakanusha.
Mzozo kwa kiwango kikubwa umesababisha kukwama kwa utafutaji wa gesi asilia na mafuta katika ziwa Nyasa.
Mwaka jana serikali ya Malawi iliiruhusu kampuni ya Kiingereza inayoitwa Surestream Petroleum kuanza kutafuta mafuta.
Habari kwa hisani ya Reuters.