HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro inakabiliwa na changamoto ya kukua
kwa maambukizi ya Ukimwi, baada ya kushamiri kwa biashara ya mapenzi ya
jinsia moja. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Naibu Meya
Manispaa ya Morogoro, Lidya Mbiaji, alisema kuwa kumekuwa na tatizo
kubwa la kushamiri kwa vichocheo vya ngono, hali inayochangia kukua kwa
kiwango cha maambukizi ya Ukimwi katika mkoa huo.
Pia alisema ongezeko la nyumba za kulala wageni nalo limekuwa kichocheo kikubwa cha kushamiri kwa biashara ya ngono zembe.
Aliionya
jamii kuepukana na mila na desturi zinazochangia kuleta vichocheo vya
kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi, ikiwemo ngoma za unyago
zijulikanazo kwa jina maarufu la kunemwa pamoja na mabanda ya kuonyesha
video ambayo nje yamekuwa yakionyesha mechi za soka, lakini ndani ya
mabanda hayo huonyesha picha za ngono na kusababisha kuleta hamasa ya
watu kufanya ngono.
Pia aliviomba vyombo vya habari kusaidia
kuelimisha jamii namna ya kujiepusha vitendo vinavyochangia maambukizi
ya ukimwi, kwani hali si shwari kutokana na makundi ya watu wanaofanya
biashara ya ngono kuvamia Manispaa ya Morogoro.
Alisema hata kwa
wasomi wa vyuo vikuu, hali pia si shwari, kutokana tafiti kuonyesha kuwa
wana kiwango cha juu cha kufanya ngono zembe, hivyo kulitisha taifa
kupoteza wasomi wake mara baada ya kumaliza masomo yao.
“Kumekuwa
na makundi makubwa ya jamii yanayoingia katika hatari ya kupata
maambukizi…ukiangalia kundi la wanafunzi, watu masikini na wanawake,
hasa wajane changamoto hii inawagusa moja kwa moja,” alisema Mbiaji.
MAPENZI YA JINSIA MOJA YADAIWA KUSHAMIRI HALMASHAURI YA MOROGORO
0
June 16, 2013
Tags