Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack
Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi
huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani
imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini
ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama
itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia
ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa
ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa
zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na
nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama
atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga
kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile.
Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya
‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika
nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la
Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni
karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa
kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa
Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za
kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali
maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi
atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote
itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani
zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi
ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo
linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais
Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland
Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi
za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari
Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya
Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye
msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia
maji ya chupa zaidi.
“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu
wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,”
ilisema taarifa hiyo.
Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria
nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na
kupuliza inayoitwa Deet.
Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti
ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani
kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na
raia mwaka 1957.
ATM nazo noma
Pia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama
wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko
karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri
kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi
watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo
zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye
vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya
mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo.
ina maana nasis kikwete akienda ulinz unakuwa mzito hvyo?
ReplyDeleteKikwete akienda marekani hata hakuna anayeshituka zaidi ya balozi wetu. Ni kama sisimizi akipita barabarani.
ReplyDeleteHahahaa looo raisi wa Dunia
ReplyDeletelabda akienda arushaaaaaaaaaaa
ReplyDeletedah hawa wa2 noma.kama kwa rais ni hivi je kwa mfalme ?.
ReplyDeleteSIONI TIJA YA HII ZIARA
ReplyDeletesure
DeleteThis comment has been removed by the author.
Deleteacheni ufala waTanzania...Obama si MUNGU!
ReplyDeleteda.............,
ReplyDeletejamani,alie juu yupo juu tu,
huyo anaesema anachukia americans just hizo ni propaganda zake ili nae aonekane,
south africa pamoja na umafia wao wamefyata,
ije kuwa sisi,
tuongee tusiongee,ratiba ipo pale pale.
hata wangekuwa kina HAO kama alivosema kakangu ,wangefyata tu
Maraisi wawili kwa mkuupuo so mchezo .Bush ni Rais na Pia mtoto wa rais
ReplyDeleteSafi sana kennytapawazi, sioni kinachofanya watu watoe maneno ya husda. Wa 2 havai moja hiyo itabaki kuwepo so kubalini matokeo. Ratiba ya ulinzi na usalama wa ziara iko palepale.
ReplyDelete2+0 = 20
ReplyDeleteSawa Haina shida atakama mneifuta comment yangu. Lakini Na nyie muwe wazalendo Au Ndo mnaogopa ukweli! Obama hajui Kiswahili Na ata JK akiziona izi comment hafanyi lolote.
ReplyDeleteIvi Obama anakuja kufanya niñi Tanzania ? Je wamarekani wameooteza kiasi gani kwaajiri ya ziara yake ? Jiulize Na wewe. Watanzania tumekua tukiishia kushanikia kuja Kwa maraisi wakigeni nchini Mwetu huku hatujui kichafanyika huko ikuru Ni nini, hebu tasmini Ni mikataba mingapi yakisilisili imesainiwa? Watanzania tunatumia nguvu nyingi sana kutafuta kipato Kwenye ardhi yetu huku wachache walio wabinafsi wakila kiulaiiiiiiini Kwa mikataba yakisirisri Kama igwatavyo. Haya bwana kazi Ni Kwako 'Karibu mgeni mwenyeji niumie' nakupenda Tanzania
ReplyDeleteah muna gas asilia nyny ndo mana atakuja kila raic mcjal na misaada itazd ili wakitaka gas muwape kwa bei ya buree
ReplyDelete