Hata uko pekee yako unawasha indiketa tu.
Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, 3 na O/D.
Kwanza ujue kabisa katika hali ya kawaida gari yako inapaswa kuwa katika D kwa maana ya Drive na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali yali ya hewa kama ni nzuri ila 2, 3 hutumika tu pale unapokuwa either unashuka au unapanda mlima/mteremuko mkali sana na mrefu mf’ sekenke na unataka ushuke au upande kwa speed ile ile ila isizidi 40/60 basi ndo unaruhusiwa kutumia 2, 3. Namba 2, 3 na L inamaana kuwa ina inalock gear box ili gear zisibadilike (-/+) kama ambavyo zinabadika ukiweka D na itambulike kuwa unaweza kubadili toka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe speed zaidi ya 40/60 maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani (disks) zilizomo ndani ya gearbox kufanya gazi nah ii upelekea ile hydrolic iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha gear box kutokuwa na nguvu ile ile (constant velocity) na ndo maana ukiweka 2, 3 au L gear box inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani/disk moja tu kwa hiyo inasaidia ile hydrolick kupoa pia na ndo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla. L inatumika pale unapokuwa either umekwama au unavuta gari jingine au tera ila inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana inanguvu sana na pia inaongeza ulajo wa mafuta, so kama ukiishatoka katika mkwamo na unaona bado barabara si nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka 2 au 3 na wakati huohuo unaweza kuweka hata D kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau speed 40/60 au zaidi kama utaweka D. kwa maana rahisi zaidi kwamba 2,3,na L inafanya kazi kama gari ya Manual nah ii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.
Over Drive inatumika pale gari inapokuwa speed zaidi ya 60/80 kutegemeana na aina ya gari na hili hutokea bila wewe kujua maana gari yenyewe ndo inafanya nan do maana unashauriwa iwe on muda wote kusudi gari ichague ni wkati gani iweke on au of maana uukiwa chini ya 60/80 hata kama umeweka on bado inakuwa haifanyi kazi.
Cha mwisho ndugu zangu ni kwamba OD unaweza kuitumia kama break/stop engine hasa unapokuwa zaid ya 80 na wakati huo iko ON yaan katika dashboard taa ya OD izime ikiwaka maana yake iko OFF, basi ili upunguze mwenda kwa haraka unachofanya ni kuweka OFF na wakati huo unakanyaga break taratibu utaona mwenyewe gari lako linavyopunguza mwendo tartibu na wakati mwingine si lazima ukanyage break, we iweke OFF tu halafu toa mguu katika pedal ya mafuta gari lazima li slow down na kama lilikuwa ni tuta na umeliisha lipita basii iweke tena ON ongeza mafuta auu unaweza kuweka 2 au 3 ili gari ianze kwa kasi zaidi na ikiisha changanya basi rudi kwenye D na endelea kama kawaida.
Tahadhari: never ever kata kona wakati uko speed kubwa na gear namba tano (Kwa manual) au rpm iko 3000 Kwa automatic hii husababisha kupitiliza maana gari inakuwa nyepesi sana. Hakikisha ume slow down mpaka gia namba nne na break kidogo na Kwa autimatic either uweke 2 au 3 ila lazima weka OD off na break kidogo
Sijui kama ntakuwa nimeeleweka maana Kiswahili na lugha yetu ila mmh …!
Jombaa umetisha mzee sabu double indicator watu wanatumia tu bila ya kujua. Tena nafikiri hata baadhi ya maafisa usalama barabarani hawalijui hili suala. nafikiri tujaribu kufanya kwa vitendo kwenye cross road afu tuone nini kitatokea.
ReplyDeleteKuwasha indiketa ya kushoto ni lazima pale unapomaliza kumpita Dereva wa mbele yako, mtoa mada pia lijue hilo usiseme sio lazima. Lengo la indiketa ni Taarifa Dereva mwenzako hawezi kujua lengo lako inawezekana umempita ili uingie barabara ya kulia sasa ili ajue lengo lako ni kumpita na kuendelea na safiri moja lazima umtaarifu kwa indiketa ya kushoto kwamba unarudi uelekeo wa kushoto.
ReplyDelete