"MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA ULIPANGWA NA CHADEMA WENYEWE".....NAPE NNAUYE

Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22) -kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.

Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.

Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka.


 Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.

Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.

CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio hilo.

Ni vizuri serikali ikalichunguza swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa, inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.

Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha.

Aidha kauli za kukata tamaa za viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili lilipangwa na Chadema wenyewe.

CCM tunaendelea kusisitiza na kulaani juhudi za wenzetu kujaribu kujenga umaarufu wa chama chao juu ya damu za Watanzania. Juhudi hizi zinapaswa kulaaniwa na wazalendo wote ndani na nje ya nchi.


 Tukumbuke asiyekubali kushindwa, si mshindani. Si busara wala uungwana na ni kinyume na utu kutumia majanga ya kutengeneza kama mtaji wa kisiasa.

Lakini CCM tunalaani pia kitendo cha viongozi wa Chadema kujaribu kutumia baadhi ya misiba na majeruhi wa tukio hili kisiasa na mwisho wa siku kwenda kuwatelekeza hospitali baadhi yao baada ya kuwaahidi kubeba gharama zote za matibabu na mazishi.

Tunaipongeza serikali kwa kuingilia kati na kuwasaidia waathirika hawa na kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.

CCM inarudia kueleza masikitiko yake kwa waathirika wa tukio hili la kinyama na kikatili lisilostahili kuvumiliwa hata kidogo.

Kama Chama tumeguswa sana na tukio hili pamoja na kulilaani, tunawasihi watanzania tushindane na kutofautiana bila kupigana na kuvunja tunu ya nchi yetu ya amani na utulivu.

Katika demokrasia ya vyama vingi swala la kuvumiliana ni swala la msingi sana katika kufikia ukomavu wa demokrasia hiyo.

Imetolewa;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi.
17/06/2013

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naamini Nnape anajua mdomo unaweza kusababisha maafa ya namna gani.. Kama una uhakika na aliyepanga matukio haya kaeleze vyombo vya dola washughulikie hao watu. Usiendelee kumwaga mafuta kwenye moto. Raia hata wakiichukia chadema usifikiri wataipenda ccm.

    ReplyDelete
  2. Naona jamaa anajaribu kukisafisha chama kwa porojo zisizo na mantiki,Nape jipange upya kusafisha chama sababu bado raia hatujakuelewa.

    ReplyDelete
  3. Tutafute aliefanya tendo hilo sio kunyoosha vidole au kuingiza siasa maana na Tukio la kanisa olasiti tutasema ni nani tusichochee tutafute suluhisho

    ReplyDelete
  4. Watu hawana imani na CCM yaani CCM imekuwa majambazi, magaidi na kadhalika na huyo Nape na Upara wake kama Rooney huo na miguu imepinda kama Upinde wa kikoloni afunge domo lake kama kilema bwana....arghhhhh

    ReplyDelete
  5. wao wanajiwahi kuwa chadema wamejilipua wenyewe.mbona chadema hawajasema ccm ndio wamelipua.ni km alikuwa anajua kitakachotokea akajipanga kusema vile.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We upo nchi gani mbona mbowe ashasema ni CCM na polisi na serikali ndo wahusika,nape yupo anamjibu

      Delete
  6. Mpuuzi we nape,umefilisika kichwani,tumekuchoka na huyo mpuuzi mwenzio Nchemba,useless

    ReplyDelete
  7. kweli nape umedhihirisha upuuzi wako.kweli wanaweza kupanga kujiuwa wenyewe
    hii inaonyesha jinsi gani viongozi wa ccm mlivyo kuwa hamna busara,ndugu yangu nape hata ukitia chuki watu waichukie chadema ni kazi bure ,tumefunguka kaka mtatoka hata kama siyo 2015 ila juwa tumewachoka

    ReplyDelete
  8. instead of pointing fingers, be part of the solution

    ReplyDelete
  9. Elias

    Nape, you should stop your stupid comments before Tanzanians. Wewe kwa akili zake za kitoto utaamini kwamba Chadema walitaka kumuua (to kill) Mwenyekiti wa Chama Chao kwa ajili ya uchaguzi wa kata nne tu za madiwani? Unaamini kwamba Chadema walipanga kumuua Mbunge wao wa Arusha waliyempigania kushinda uchaguzi huo wa mwaka 2010? Je, unaamini Chadema wangeweza kuua wanachama au wapiga kura wao wenyewe? Acha kuwadanganya Watanzania. Wewe Nape ni mpuuzi tena usiye na busara wala utashi wowote. Pesa mnazoiba kupitia CCM zinawapotosha, hata Mwenyezi Mungu ameamua kuwanyima busara za kuzungumza na Watanzania. Mafisadi wakubwa nyie! Wewew tunakujua. Ni mtoto wa malaya!

    ReplyDelete
  10. Sifanyi siasa wala sipendi siasa ila naona chadema na CCM wote mnaleta fujo tanzania hamna la maana hasa chadema ndo keroooooo wakifatiwa na CCM,we uikombie nchi inakuhusu nini we jikomboe wewe au hutaki si uhamie rwamba au congo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad