Huyu ndiye Carol aliyempa Breezy nguo yake ya ndani |
Wakati Chris Brown yuko jukwaani anatumbuiza katika show ya Anaheim Jumamosi usiku (June 22), shangwe za kutosha zilisikika muda wote wa show na ghafla kuna binti aliyekuwa karibu kabisa na jukwaa alifanya kila awezalo kupata attention ya Breezy, kisha akamkabidhi nguo yake ya ndani (thong) hapo hapo jukwaani .
Inashangaza sio? Chris aliipokea nguo hiyo kwa mshangao, akaitazama kisha kuiweka chini na kuendelea na show.
Akizungumza na TMZ msichana huyo mrembo aitwaye Carol Quiroz amesema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa CB hivyo mpango wake ulikuwa mmoja tu, alikosa njia ya kuweza kuongea na Chris hivyo aliamua kuchukua nguo yake ya ndani na kwenda kumpatia.
Plan ilikuwa sio kumpatia tu nguo ya ndani, lakini aliiandika jina lake, namba yake pamoja na mawasiliano ya Instagram kwa kutumia marker pen kisha akampatia Chris akitegemea kupigiwa endapo ataona mawasiliano hayo kwenye nguo hiyo. “I wrote my name, number and Instagram on the thong in permanent marker. I got his attention and handed it to him.” Alisema.
Carol aliongeza kuwa nguo hiyo ilikuwa ni mpya haijatumika na aliingia nayo club akiwa ameiweka katika ‘bra ‘ yake.
Pamoja na juhudi zote hizo binti huyo alisema Chris brown bado hajawasiliana naye mpaka sasa!
Tazama video wakati Breezy anaipokea nguo hiyo ya ndani kutoka kwa msichana huyo
Source:Bongo 5