MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja
mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab
(30). Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya
Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita. Akizungumza jijini Dar
es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema
mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia
takataka maeneo ya Mikocheni B.
“Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupia taka Mikocheni ‘B’,
katika eneo linalomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
“Mfanyakazi
huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu
ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha
kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za
kichwani,” alisema Kova.
Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye
alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku
hiyo ya Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu.
Alisema baada ya polisi
kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha marehemu na
nguo alizovaa siku ya tukio, ambazo zilikuwa zimetapakaa damu.
“Nguo hizo za marehemu zilikuwa zimetapakaa damu na baada ya mahojiano ya muda mrefu, mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kamishna
Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa marehemu alitoweka
nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi mtuhumiwa
alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kova alisema mtuhumiwa bado anahojiwa na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Muuaji wa Dada Aliyechinjwa Mikocheni B Apatikana
0
June 12, 2013
Tags