MWANA FA..AJUTA KUANZISHA BIFU NA JIDE,,APOTEZA MASHABIKI,HANA RAHA AAMUA KUFUNGUKA..SOMA ALICHOKIANDIKA HAPA


Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.


Mwanamuziki Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake
kuna jina la Jay Dee.

Tofauti na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.

Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.

Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.

Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.

Source:The Choice Blog

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuwa na jina kubwa kusikufanye ukawaona wengine hawafai au kusikufanye ukatengeneza dharau kwa wengine na kujiona kwamba wewe umemaliza na kila utakachokifanya watu watakusapoti SIO, kuwa na jina kubwa vilevile i kuwa karibu na watu na kujaribu kufanya kile kitakachowafurahisha watu bila kubaguwa huyu ananipenda na huyu hanipendi... TAKE CARE MDOGO WANGU FA. "...TUPENDANE SISI KWA SISI KWANZA ILI KUWASHAWISHI WENGINE WATUPENDE...".

    ReplyDelete
  2. Siku zote usipende kuendekeza shida,FA Mtafute ANACONDA Mwangukie huo ndio ustaarabu

    ReplyDelete
  3. Ingelikuwa amutafute Jide kisha wapange show myingine wako pamoja.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad