Jambo hili
huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu
mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale
wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu
baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.
Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni
katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni
maumbile.
Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa
wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la
kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa
jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la
kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata
usingizi.
Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki
wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali
lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama
scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale
wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na
kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.
"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.
“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.
Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na
jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala
baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….
Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya
kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu,
watuwache tupumuwe……
Source: Jamii Forums
sasa mnawasaidiaje hao wanaume wa aina hiyo, wafanye nn kutatua tatizo la kuchapa kiseto baada ya kujamiana?
ReplyDelete