MWENGE KIMENUKA , POLISI NA MGAMBO WA JIJI WASHIRIKIANA KUPAMBANA NA WAMACHINGA

Leo jioni wakati natoka katika shughuli zangu nilipita maeneo ya Mwenge pale stand ya mabasi nimekuta kweupe wale vijana wanao uza nguo kwa kupanga chini na kuzishika sikuwaona ...nikauliza nikaambiwa wamefukuzwa kwa ajili Oboma Anakuja...Mmhhh Kazi kweli kweli ...
Wakati bado nashangaa shangaa Mara likaja gari la Polisi na Wale mgambo wa jiji...Mara nikaona watu wanakimbia huku na kule ...Kushangaa kumbe wale wamachinga bado wapo ila wanauza kwa kujificha ficha kwenye vichochoro vya maduka..Sasa Kimbembe kikaanza wale wanamgambo wakawafuata huko huko na kuanza kuwapiga na kuwavunjia meza na viti vyao...Kwa kweli iliniuma sana kuona watanzania wenzetu wakifanyiwa hivyo ....Bado sijapata jibu ...siko zote mbona hawakufukuzwa ?? Huu Ugeni ndio imekuwa Nogwaaaaa....Na uhakika kuna ambao wanalisha na kutunza familia kwa kazi hizi za umachinga sasa watakula wapi kama hali ndio hiyo????

By Regina Iwole

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii ndo tanzania ya wanyonge kuonewa,mji ausafishwi had aje rais wa dunia?,baada ya mgeni aje wenyeji wapone sasa mgeni aje wagen wasulubiwe,

    ReplyDelete
  2. shame on you TZ gov't, hata mungu hammuheshimu kama hvy, lkn mnathamini sana kiumbe chake mpaka mnasababisha kudhulumiana, Obama si chochote kwa mungu, Mungu atawaongoza wote waliodhulumiwa, ameen!!!

    ReplyDelete
  3. Hao viongozi na hiyo Halmashauri ya sijui Jiji woote ni WAPUMBAVU. Wanafikiri hao wageni hawajui yanayotendeka humo ndani ya nchi? Siku hizi kuna Satellite kila kona inaona na mtu yeyote haaswa wale waliopo nje hitumia saana kuangali majumbani kwao .... chagueni viongozi wanaoendana na wakati na sio washamba washamba, wengine washamba hata wa nguo za kuvaa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtu hunena kilichoujaza moyo wake, lugha kali simsaada. wapeni heshima wanaostahili heshima na kutetemeka wanaostali kutetemeka. hivyo ndivyo neneo la Mungu linavyosema

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad