Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa
aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa
wabunge.
“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja
na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.
“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari,
halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama
kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo,
Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni
kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.
source gazeti la mwanainchi leo.
Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge
hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na
spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam
Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini
Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.
Naibu Spika Ndungai Apinga Vikali Spika Kutokuwa Mbunge
1
June 05, 2013
Tags
Huyu ndugai hana akili. Huwezi kufananisha madaktari na wabunge. Udaktari ni taaluma inayomghalimu mtu si chini ya miaka mitano ya kuosomea. Ubunge ni swala la mtu kuwa na umri wa miaka ya kuchaguliwa tu. Hakuta utaalamu wowote wa kuwa spika.. Tunataka mti asiye na chama ili kuwe na usawa na haki bungeni.. Tatizo ccm wanaogopa kupoteza nguvu ya kukandamiza upinzani bungeni.. Kuhusu kama inafaa au haifai spika kutokuwa mbunge tuache sisi wananchi tuamue katika kura za maoni. Sio wewe.
ReplyDelete