Rapper Nay wa Mitego ni miongoni mwa wasanii waliojitokeza kulaani kitendo cha gazeti la Ijumaa lililoandika habari ya kumchafua Ommy Dimpoz kiasi cha kumfanya achukiwe na mashabiki wa muziki. Gazeti la Ijumaa liliandika kuwa Ommy alimtukana Mangwair kwa kudai kuwa alikufa maskini.
Nay Wa Mitego ameandika kupitia kurasa za Facebook na Instagram kuwa ameshindwa kuvumilia kwa kile kinachoendelea kwa mashabiki wa muziki kupoteza matumaini na upendo kwa Ommy Dimpoz ambaye wiki iliyopita alipondwa na makopo ya bia kwenye show ya Kili Tour mjini Dodoma.
“Nimesikitishwa sana na vitendo na shutuma zinazoendelea dhidi ya msanii mwenzetu OMMY DIMPOZ nimeshindwa kuvumilia inabidi niongelee hili swala Kama Ulifatilia kwa Makini alichokisema OMMY siku ya usiku wa tunzo za Kili Alisema Makampuni Makubwa yawekeze kwa Wasanii kwa sababu kazi tunayofanya ni kubwa lakini matokeo yake tunakufa Masikini…Lakini kuna watu kwa sababu zao binafsi wameamua kupandikiza Chuki kwa Kumtumia Marehemu ALbert Mangwea ili kumuharibia DIMPOZ maisha yake ya kimuziki.Watanzania tufungue Macho sio kila kinachoripotiwa kina ukweli Mnaweza kumuhukumu Mtu asiyekuwa na Hatia kisa kuna watu wametumia Mamlaka na Power zao kuangamiza wasiokiwa na Hatia Kwa maslahi yao Binafsi…..Ina maana Ndugu zangu Mnapenda wasanii wenu Tuendelee kubaki na kufa Masikini wakati kazi tunayofanya ni Nzito….Ni hayo tu,” aliandika Nay.
Neema wa mitaego acha kumtetea hyo bwenge pumbavu we....
ReplyDeleteUyo ndo dada neema buana!
ReplyDeleteUpeo wa kufikiri ni kitu kikubwa sana, ukifikiri chini hata maamuzi yatakuwa chini! Kwanini watu wasiwe na uwezo wa kuhoji!? Haya ndo matokeo, kila mtu awe na busara na is vibaya nmtu kuita koleo koleo na kijiko, kijiko
ReplyDeleteKweli gazeti la Ijumaa lilichemka kama sio kufanya makusudi kabisa. Maanake alichoongea Dimpozi wala hakikuwa na utata wowote. Yeye alitakiwa apongezwe kwa kuwatetea wasanii sio kulaumiwa. Nadhani ni kutokana na kutopewa nafasi ya kuuelezea umma wa Watanzania waliopotoshwa na gazeti la Ijumaa ndio maana maskini akaamua kuomba msamaha kwa kulazimishwa na mazingira. Dimpoz hakutakiwa kuomba msamaha kabisa..aombe msamaha kwa lipi? hakuna alichokosea.Hakuna jina la msanii aliyemtaja kama amekufa maskini. Hivyo kama ni kuomba msamaha labda angewaomba wasanii wenye majina ambao walikufa wakiwa matajiri. DIMPOZ NI MPIGANIA HAKI ZA WASANII ambao wameendelea kuwa MASKINI wakati wasambazaji na wachakachuaji wanajineemesha bila kuvuja jasho. HEKO OMMY DIMPOZ, ALUTA CONTINUA! Mwandishi wa Gazeti la Ijumaa ndiye anayetakiwa kuomba msamaha kwa kuwapotosha Watanzania kwa sababu anazozijua yeye, inawezekana hajapendezwa na mafanikio aliyopata Dimpoz.
ReplyDeleteAluta ya nn tako ww unakurupka 2 kuandk kma mmeo dimpozz alivykurpka kuongea kwa kujiona yy anakisima cha hela
ReplyDeleteAluta ya nn tako ww unakurupka 2 kuandk kma mmeo dimpozz alivykurpka kuongea kwa kujiona yy anakisima cha hela
ReplyDeleteOmmy dimpoz... Aliongea ukweli... Tuwasapoti Wasanii wetu ... Wasife Masikini....Kazi wanayofanya ni kubwa.
ReplyDeleteWatanzania hawapendi kuambiwa ukweli. Ni Ngwea alikuwa ni msanii mkubwa ila hakuwa na pesa. Tujifunze kwake na tukomeshe unyonyaji. Wasanii waneemeke.
Kwan unasema alikufa masikini je account yake uliiona ina shilingi ngapi au coz michango ya kumsafilisha ndiyo mnaona masikini mtu masikini unamjua wewe
ReplyDeleteukiambiwa wewe ni maskini wakati ni tajiri, je hilo ni tusi .....! inakera kuambiwa kuna mtu amemtusi marehemu Ngwair afu kumbe ni hila tu za mtu flani...
ReplyDeleteupeo wa kuelewa ukiwa mdogo ni tatizo sana
ReplyDelete