Barani Afrika mchezo wa soka umetawaliwa na fitna pamoja na mbini
chafu ambazo hulenga kumdhoofisha mpinzani hasa kwenye mechi za ugenini
ili kutoa faida kwa timu ya nyumbani kupata ushindi kiwepesi .
Hali
hii imedhihirika kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu kwa kombe la
dunia kwa kanda ya Afrika kati ya Nigeria na Kenya ambapo timu ya taifa
ya Nigeria imegoma kutumia maji ya kunywa ambayo wamepewa na viongozi wa
shirikisho la soka la Kenya ambao kimsingi ni wenyeji wa timu hiyo ya
Nigeria .
Kocha wa Mabingwa hao wa Afrika Stephen Keshi alikataa
kupokea maboksi 25 ya maji ambayo yaliletwa na kiongozi wa shirikisho la
soka la Kenya ambapo alisemakuwa hawahitaji maji hayo na kama
wangelazimishwa kuyapokea angewaagiza wachezaji wake wayamwage .
Kitendo
hicho kiliwashangaza viongozi wa Fifa waliofika kwenye uwanja wa
Kasarani jijini Nairobi ambao walishindwa kuelewa sababu za msingi za
kocha huyo kugoma kupokea maji ya kunywa .
Timu ya taifa ya
Nigeria inacheza na timu yataifa ya Kenya huko Nairobi baadae hii leo
kwenye mchezo muhimu wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2014.
Shenz type! Wasioge pia kama kunywa hawataki! Nonsense stupid ugly creatures! Nkt!
ReplyDelete