PICHA ZINGINE ZA SHOW YA LADY JD, AOGA FEDHA, SUGUU NA PROFESA JAY WANG'AA JUKWAANI
2Udaku SpecialJune 15, 2013
Na Mahmoud Zubeiry,IMEWEKWA JUNI 15, 2013 SAA 11:00 ASUBUHIONYESHO
la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kutimiza miaka 13
katika muziki, limefana usiku wa kuamkia leo katika eneo la maegesho ya
magari kwenye ukumbi wa Nyumbani, Lounge, eneo la Kinondoni, Dar es
Salaam kwa mamia kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana
ikawa taabu.Watoto wa mjini wanasema ilikuwa funika bovu- ndiyo shoo hiyo ilikuwa nzuri mno, ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake.
Jide akikumbatiana na Profesa Jay
Jay akipagawisha
Jay akisema na nyomi
Mzee Kitime akimpiga picha Komando Kalala wakati anaimba
Komando Kalala na mkewe jukwaani
Msanii Mango Star na nyoka
Mango Star na nyoka
Wasanii
nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na
kundi lake wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha
kuiongezea utamu shoo hiyo.Kufika
saa 3:00 usiku tayari Machozi Band inayomilikiwa na Jide ilikuwa
jukwaani kuanza kutumbuiza kabla ya kumpisha rapa Wakazi kutoka Ukonga,
baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi.Saa
5:00 usiku, Jide akapanda jukwaani na kuibua shangwe nzito kutoka kwa
mamia waliokuwa wamefurika katika eneo hilo. Jaydee alianza na wimbo wa
Nilishakuwaga na Wangu, baadaye akaimba Nakuhitaji, Moto, Mambo Bado,
Yeye, Malaika, Siri Yangu, Wanock Nok kisha kumalizia na Single Boy
katika awamu ya kwanza.Baada
ya hapo, Jide akasema ilipotimu Saa 6:00 usiku ameingia katika mwaka
mpya tangu azaliwe hivyo mashabiki wakamuimbia ‘Happy Birth Day’ kisha
akateremka kwenda kukumbatiana na mama yake mzazi, Martha Mbibo na kumpa
zawadi ya fedha zote alizokuwa ametuzwa jukwaani.Jide
alirejea jukwaani na kuimba kwa ufupi nyimbo alizowahi kurekodi na
wasanii Man Ngwair na Langa Kileo ambao hivi sasa ni marehemu, kabla ya
kumpisha Mh. Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu ambaye aliimba nyimbo tatu tu,
lakini alisisimua mashabiki ile mbaya.Sugu alianza na Hakuna Matata akimshirikisha Mkoloni, Sugu na kumalizia na Mambo ya Fedha ambao ulimrejesha jukwaani Jide.Kutoka
hapo, ikawadia zamu ya Wanaume Halisi kutoka Temeke, wakiongoza na Juma
Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ambao nao walifanya balaa vile vile na
kuurusha umati ile mbaya.
Msanii M2 The P akizungumza jukwaani
KR Mulla
Sir Nature
Nature na Doro
Sinta akimpiga picha Nature
Wakati
Nature anaimba, mpenzi wake wa zamani Christine Manongi ‘Sinta’ alikuwa
bize kumpiga picha ‘mzee’ wake wa kitambo, kiasi cha mmoja wa viongozi
wa kundi hilo, Kiboya kupora kipaza sauti na kutamka Baba Sinta
akimtania Nature, jambo ambalo liliwafanya watu washangilie. Nature
kabla ya kuanza kuimba alimpandisha jukwaani msanii M 2 P aliyezushiwa
kifo wakati akiwa amelazwa Afrika Kusini sambamba na Man Ngwair. MP
alisalimia na kushukuru kwa dua za Watanzania wakati akiwa taabani
wadini, kwani zimemponya na akatumia fursa hiyo kumuombea swahiba wake
Ngwair apumzishwe kwa amani peponi.Ndipo
Wanaume wakaanza vitu vyao, wakipiga nyimbo za Sonia, Hakuna Kulala,
Mzee wa Busara, Ladhia, Haipotei, Dance With Me na Jimwage.
Jaydee na mama yake
Jaydee akikusanya fedha alizotuzwa
Anaziweka kwenye boksi kabla ya kweneda kumpa mama yake. Alyeshika boksi ni King Kiboya
TK wa M Band...
Maeneo kama haya Mh Sugu huwa si mkali...anajua kutabasamu
Rapa kutoka Ukonga
Alikuwepo...Mgaya Kingoba Mhariri wa Michezo gazeti la Habari Leo
Kutoka kulia Baraka Msilwa, Francis Kifukwe na mkewe
Wanaume
walipoondoka akaibuka msanii mcheza ngoma za asili huku akichezea
nyoka, Mango Star ambaye aliwaacha watu midomo wazi pale alipokuwa
akimnyonya nyoka upande wa kichwani. Akafuatia mkongwe Komando Hamza
Kelele ambaye kwanza alimpandisha mkewe, Stella John Momose Cheyo
jukwaani kumtambulisha, kisha akaimba nyimbo na Tumetulia.Ikawadia
zamu ya Profesa Jay, ambaye aliimba Joto Hasira pamoja la Lady Jaydee,
baadaye, Teja, Yahya na Joto tena. Jaydee akateremka na kumuacha Jay
amalizie shoo naye akamalizia vizuri kwa nyimbo za Hapo Vipi,
Nikusaidiaje na Kamili Gado.Watu
kadhaa waliofika Nyumbani Lounge kushuhudia shoo hiyo walilazimia
kugeuka na kuondoka kwa sababu ukumbi ulikuwa ‘umejaa na hakuna pa
kukanyaga’.Kwa ujumla shoo hiyo ilipendeza, ilikuwa bab kubwa.
tunakupenda sana jide mungu akupenguvu zidi ya wasiopenda maendeleo yako
ReplyDeleteJide wewe ni mkali tu dada yetu aminia kwenye gemu kitambo na bado upo juu achana na wajinga hao wanaosemasema hawakuwezi ng'oooo
ReplyDelete