Heshima kwenu wale wote mnaotumia muda wenu na
akili zenu kuwajuza wananchi. Ningependa kidogo muelewe
na ntaweka baadhi ya vithibitisho kutoka vyanzoa mbalimbali
nini hasa ni sababu ya safari hii.
KWANZA:
Yapata miaka 3 iliyopita bara la ulaya na America yalikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi
na kuporomoka kwa mabenki na makampuni kadhaa. Jambo hili lilichangiwa kwa kiasi kikubwa
na bidhaa za kifedha (Financial products) ambazo ni aina mpya ya wizi na uchotaji wa mabilioni
ya fedha. Matukio haya yaliathiri kwa kiwango kikubwa masoko makubwa ya fedha na miradi mingi
inayotegemea uwekezaji kupitia masoko hayo. Matukio haya yaliwaacha pia wawekezaji wengi wakiwa
hoi na hasara kubwa, pia ilizaa kukosa imani na uwekezaji katika bidhaa makaratasi (yaani zile
zinazoendeshwa kwa speculations na financial models) au zisizo na soko nje ya soko kuu (disposal
market). Wahanga wakubwa wa mtikisiko wa uchumi yaani MABILIONEA kwa sasa wameamua kuelekeza
nguvu zao kununu bidhaa ambazo ukua thamani kila jua lichwapo, katika hilo bidhaa kubwa na ambayo
kihistoria imekuwa ikiongezeka thamani kila siku na kwa kanuni za kikomasi -> DEMAND & SUPPLY
haitakaa iporomoke thamani.
Bidhaa hiyo si kitu kingine bali ni ARDHI, hii ni bidhaa peke duaniani ambayo huwa imebeba bidhaa
nyingi nyingi na zenye thamani kubwa (mfano: madini, wanyama, majengo, akiba kubwa ya maji safi
yaliyochini)Pia tafiti nyingi zimeonesha kuwa kutokana na ongezeko kubwa la watu duniani, inakadiriwa
kuwa ndani ya miaka 20 ijayo ardhi na maji safi vitakuwa ni adimu sana duniani. Mabilionea hawa
wameanza kumiminika Africa, sehemu pekee iliyobaki ulimwengu yenye ardhi nzuri kwa shughuli
nyingi za kimaendeleo pamoja na kilimo. Africa pia inasababu nyingine kuu ya kuvutia hawa
Mabilionea, watu wake wengi ni maskini na viongozi wake wengi wanauchu mkubwa wa pesa.Hapa chini
nimeweka linki ya dokumentari ya Aljazeera ambayo inaongelea uporaji ardhi mkubwa na pia naweka
na video ya taarifa za kiintelijensi za mikakati ya mataifa makubwa:
Uporaji ardhi: Our Man in Sudan - Witness - Al Jazeera English
Intelijensia: imeambatanishwa
PILI:
Obama ni nani??? Watu wengi wameaminishwa Obama ni rais anayeweza leta mabadiliko na atakuwa na
nia njema na Africa kutokana na rangi yake na pia kuwa na mzazi aliyetokea Africa. Hapa ndio watu
wengi na waafrica kwa ujumla walioshindwa kungamua mikakati mikubwa na ya mbali inayopangwa na hawa
mabilionea wakubwa (Capitalists) wanaotawala dunia. Mtashangaaa sana lakini, ukweli huwa ni mgumu
kukubalika vile vile kizazi chetu kinatumikishwa sana kiasi mwisho wa siku huwa akina muda wa
kuchakatua matukio na taarifa mbalimbali zaidi ya kutegemea magazeti, televisheni na blogu kuwajuza.
Ni wachache usumbua akili kuunganisha na kutafiti habari.
Dunia yetu inaendeshwa na mabilionea wachache na si serikali tunazoaminishwa kuwa zipo kuendesha
nchi zetu. Siasa kama vilivyosekta nyingine nayo iliishabinafsishwa. Obama ni chambo kilichowekwa
kuwezesha maliasili nyingi za kiafrica kupatika kirahisi bila kuhitaji nguvu ya ziada na mikakati
mizito. Je Obama ni mwafrika?? jibu lake lina utata maaana hata cheti chake cha kuzaliwa na taarifa
za mahali alipozaliwa vimejaa taarifa zinazochanganya sana. Cheti chake cha kuzaliwa kinaonesha
kazaliwa hospitali inayoitwa Kapi'olani Maternity & Gynecological Hospital, siku ya kuzaliwa ni
1961 Agosti 4, baba mzazi akiwa na Umri wa Miaka 25, mzaliwa wa nchi ya Kenya.
Lakini historia na kumbukumbu zingine zinaonesha kuwa hospitali hiyo haikuwa inatumia jina hilo
wakati Obama anazaliwa. Mwaka 1961 kulikuwa na hospitali mbili zilizojulikana kama Kapi'olani
Maternity Home na KauiKeolani Children's Hospital zilizokuja kuungana mwaka 1978 na kuanza kuitwa
Kapi'olani Maternity & Gynecological Hospital. Vile vile cheti hiko kinatamka baba mzazi ni raia wa
Kenya, lakini hakukuwa na nchi inayofahamika kama KENYA kabla ya mwaka 1963. Sehemu iyo ya Africa
mashariki ilijulikana kama British East Africa Protectorate. Kumbukumbu pia zinaonesha kuwa Obama
amewahi kuchapisha kitabu kinachohusu maisha yake na baba yake. Kwenye kitabu hicho Obama anamsifu
babayake kwa kujitolea kupigana kwenye vita ya pili ya dunia, WW II. Kwa waliosoma historia
wanatambua kuwa WW II ilikuwa kati ya mwaka 1939 na 1945. Hisabati ya haraka haraka inatuambia kuwa
mtu mwenye umri wa miaka 25 mwaka 1961 atakuwa na umri wa miaka 3 mwaka 1939 na kufikia mwaka 1945
atakuwa ametimiza miaka 9. Je, na ntaomba msaada wa wanajeshi walipigana vita hii (veterani)
watueleze kama na watoto wa miaka 3 walienda vitani kipindi kile au hata wala wa miaka 9 walikuwa
mstari wa mbele pia. Tunatambua kuwa mkoloni aliswaga watu wote waliokuwa na nguvu na kuwapeleka
vitani na kwenye mashamba yao, huku nyuma akiicha wazee, wanawake, wale dhaifu, walemavu na watoto.
Cheti hiko cha kuzaliwa kinamtambulisha mtoto kama ni wa jamii ya African-American wakati miaka
iyo raia wote wa marekani waliokuwa na rangi nyeusi waliitwa na kutambuliwa kama Negroes hadi miaka
ya 1970 mikakati yao ya kudai usawa ilipozaa matunda na kutambuliwa rasmi kama African-American.
TATU:
Wachina wameisha ikamata dunia. Tambueni ya kuwa muhimili wa nguvu za uchumi wa dunia uliishaamia
Asia. Miaka ya nyuma mataifa makubwa kiuchumi yaliungana na kuanzisha G5 baadae ilitanuka na kuwa
G8. Natumaini wote mwaelewa nini maana na makubariano ya wanachama wa G5, kimsingi haina tofauti
sana na yale yaliyojiri pale Berlin 1884 chini ya Bw. Bismarck, dhana kuu ikiwa ni kutoingiliana na
kuharibiana mikakati ya biashara zao ili wote kwa pamoja wafaidi. Waliokuwa mezani miaka ile ya
1884 walikuwa wajerumani, waingereza, wafaransa, wareno n.k Maana hawa ndio waliokuwa na nguvu
kubwa miaka ile, top 5 ya mataifa yenye uchumi mkubwa wakati huo ilikuwa ni iyo.
Kwa mlinganisho, top 5 ya leo ndio iyo G5 na imelazimika kupanuka na kuwa G8 ili kudhibiti hao watatu
wasiwapoke nafasi zao.Baada ya manyanyaso na taabu ya kujitanua, mataifa chipukizi ya Asia yaani
China na India yaliamua kutafuta mkakati wa kujikwamua kwenye makucha ya kibebure ili wapate nafasi
ya kukuza chumi zao kwa spidi kubwa isiyodhibitika na gavana za magharibi. Waliazimia kuungana na
mataifa makubwa kiuchumi na raslimali kutoka kila bara ili kuweza kuwa na msuli mkubwa. Hapo ndipo
walipozikaribisha Afrika ya kusini na Brazil. Pia ili kuweza kuhimili geo-political influence na
military muscle (samahani kwa kiingereza hapo)waliikaribisha Russia, taifa peke duniani nje ya
africa lenye utajiri lukuki wa rasilimali na ambalo linanguvu kubwa kijeshi duniani (zaidi ya Marekani).
Machache hujulikana kuhusu nguvu za kijeshi za Russia kutokana sera yao ya usiri,
na haya tuyajuayo ni kupitia mataifa ya magharibi.
Huu ndio ukawa mwanzao wa muungano wa BRICS (Brazil, Russia, India, China & South Africa) katika
safari ya kuiteka na kuimiliki dunia toka wanyanganyi wa magharibi waliowapora maendeleo na
teknolojia miaka ya 1770. Fanya utafiti kuhusu uwezo wa bara la Asia miaka iyo, nguv ya japan kule
Asia-Pasifiki, pamoja na teknolojia zilizokuwapo pale Forbiden city. China ndio taifa kubwa katika
kila nyanja ndani ya BRICS na hivyo ndio kiranja mkuu. Siku za hivi karibuni wachina wamewasha
indiketa yao na kuanza kuchomoka kwa kasi zaidi ya zile Scania za Marcopolo kule Chalinze-Segera.
Baada tu ya uongozi mpya kushika hatamu ulianza kufanya safari na makubaliano muhimu kibishara na
kiustawi na mataifa ambayo yatawezesha ustawi wao wa haraka, kwa kuanza kufunga mikataba na mataifa
yote yenye utajiri mkubwa (Tanzania, South Africa, Russia, Congo-Brazzaville) wa rasilimali
zinazoitajika kwa kiwango kikubwa China na sasa uongozi huo baada ya kuishapata uhakika wa chakula
(malighafi) chakutosha kulisha viwanda vyake, umeangia katika raundi ya pili ya kuhakikisha inapata
"masoko bila masharti" na hivyo kuanza ziara mabara ya Ulaya na Amerika na kufunga mikataba ya
moja kwa moja (bilateral) na mataifa yenye masoko makubwa (Hungary, Bulgaria, Turkey, Belgium,
Romania, German, Mexico, USA etc). Mojawapo ya safari muhimu kuliko zote ilikuwa ni ile ya nchi ya
Switzerland, ambayo inafahamika kama muhimili mkubwa wa masuala ya biashara kubwa za kifedha na
mihamala (transactions)ya rasilimali kama(mafuta & heavy metals) na commodities kama (ngano,
mchele, pamba, chai, kahawa). China imefanikiwa kuingia mikataba ya moja kwa moja na nchi hii na
kufungua ukurasa mpya wa mahusiano pamoja na kubadilisha mizani ya mtiririko wa bishara duania.
Lengo kuu la china ni kuitafuta sarafu mbadala kwenye biashara za kimataifa ili kuondokana na dola
kwenye mzunguko wa biashara za kimataifa. Kwa muda mrefu imekuwa ni agenda ya BRICS kuanzishwa
sarafu mpya ya kibiashara na kuachana na zile za magharibi (Euro & Dollar) ambazo ni dhana nyingine
za mfumo wa kibeberu. Naomba ujifunze kuhusu athari za sarafu za kigeni katika biashara yoyote.
Kwa ufupi china imefanikiwa kukubaliana na switzerland kuruhus kutumika kwa sarafu ya china katika
biashara kubwa moja kwa mojabila kubadilishwa na sarafu yoyote.
HITIMISHO:
Kwa waliomudu kutazama taarifa ya habari juu ya mkutano wa Obama na Xi, utaona jinsi Obama
alivyojawa na wasiwasi hata sauti yake ilikuwa kama inatetemeka. Pili mkutano ule haukuwa pale
Washington kama vile viongozi wengine wanapokuwa wameenda USA kukutana na raisi wa Marekani,
mkutano huu unafanyika California, eneo lilipendekezwa na Xi na watu wake. Obama na timu yake
wameitwa kukutana na Xi, na si vinginevyo,
Source:Jamii Forums
Du ngachoka kapisa
ReplyDeletemmmmmh hali tete kiukweli inahitaji jicho pevu kuona yaliyopo na kutambua yajayo
ReplyDelete