Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume
hiyo, Profesa Sifuni Mchome alisema inachunguza mfumo mzima wa elimu na
kuwa suala la Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 ni moja kati ya
mambo wanayoyafanyia kazi.
Mchome ameeleza hayo siku moja baada ya gazeti
dada la ‘The Citizen’ kuchapisha habari za kujiuzulu kwa mmoja wa
Wajumbe wa Tume hiyo, Rakesh Rajani aliyefikia uamuzi huo kutokana na
kile alichosema ni kutoridhishwa na pendekezo la kufutwa kwa matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne.
Alisema ripoti ya Tume hiyo itakayowasilishwa kwa
Waziri Mkuu, Juni 15 mwaka huu, imebaini mambo mengi ikiwa ni pamoja na
mitalaa kupitwa na wakati pia idadi ya wanafunzi kuwa kubwa na kuelemewa
kwa mfumo wa elimu nchini.
“Kuna mambo ya kuangalia ubora, kuna suala la
ofisi na taasisi mbalimbali zinafanya kazi gani? Vipi uwajibikaji wake,
majukumu yake na mgawanyo ukoje, Ofisi ya Kamishna inahusika vipi na
mitihani, huku kote tumeona kuna matatizo,” alisema.
Alisema pia morali ya walimu imeshuka, jambo
linalofanya wengi kuwa tayari kuachana na kazi hiyo wakipata jambo
jingine la kufanya.
“Wengi morali imeshuka, wangepata nafasi ya
kuchoropoka (kuondoka) wangekimbia, lugha ya kufundishia ni tatizo na
mchango wa wazazi kwenye elimu ni wa kuangalia, yote haya ni matatizo,”
alisema.
Alisema kuna haja ya sera mpya ya elimu ambayo imekuwa ikizungumzwa tangu mwaka 2008 ili kutatua matatizo yaliyopo sasa.
Akizungumzia kujiuzulu kwa Rajani, alisema sababu aliyotoa haina msingi kwani muda mwingi hakuweza kufanya kazi na tume hiyo.
“Rajani ushiriki wake kwenye tume ni chini ya
asilimia 10, muda mwingi alikuwa anasafiri au anakuwa kwenye kazi za
asasi yake, mambo mengi alikuwa hajui na sisi tulikuwa kila kitu
tunaamua kwenye vikao, kuna kazi tuliyompa ya kuangalia kama kila
tulichojipangia kimefanyika kwa wakati, alishindwa kwa sababu muda
mwingi hakuwapo,” alisema:
Alisema kuwa, msimamo wa Rajani ulikuwa ni
kuachana na wanafunzi waliofeli na badala yake tume ijikite kuangalia
mambo mengine, jambo alilosema lilikataliwa na wajumbe wengine.
“Sisi tuliona kuwa ni ukweli mfumo uliotumika
kupanga matokeo ulikuwa tofauti na kukaonekana kwamba ukibadilishwa
matokeo yatakuwa tofauti, ndiyo maana tukasema matokeo yapangwe upya.
R.I.P ELIMU TZ
ReplyDeleteWanauza kuma hao au
ReplyDelete