Uchambuzi wa video mpya ya Ben Pol ‘Jikubali’ iliyotengenezwa na Nisher


Video ya wimbo mpya wa Ben Pol, Jikubali imetoka rasmi leo. Video hiyo imefanyika jijini Arusha na kuongozwa na kutengenezwa na Nisher. Video imepokelewa vizuri na watu wameendelea kuisifia. Huu ni uchambuzi wangu kuhusiana na jinsi nilivyoiona video hii.
1. Muendano wa picha za video na muziki wenyewe (Relevance of Visual Images To Music)

Japo si kitu kibaya kwa muongozaji wa video hii kutumia mhusika mmoja kwenye video mwanzo hadi mwisho, wazo na maudhui ya wimbo kama Jikubali yangependeza zaidi kama yangesaidiwa na baadhi ya picha za watu wanaotajwa ama vitu vinavyozungumzwa. Najua ukitaka kufanya video ya aina hiyo basi lazima ugharamike zaidi lakini Jikubali haikuwa video ya kukosa picha za ziada.

Kwa mfano katika sehemu anayotaja majina ya watu kama Mwana FA, AY, Khadija Mwanamboka, Salama Jabir, Hasheem Thabeet, Linah, Shaa, Diamond, JB, Ray, Lady Jaydee. Video ingekuwa tamu sana kama picha zao zingeonekana wakati akiyataja majina yao. Ingewezekana kabisa kwa Nisher na Ben Pol kupata picha fupi (za video) za watu hawa na tena bila kuwalipa chochote.

Herson Alawison naye ameliona hilo na ameandika: KWA MABORESHO ZAIDI NEXT TYM- atleast ungeweka clip za watu wanaotajwa na Ben au picha kuonyesha how they can inspire jamii itake kuwa kama wao…ungemtupia Jakaya pale kati…m2 kama Jide, Zito n.k. ni ushauri 2 bra ili kazi zetu zisimame zaidi maana ukifanya video wewe naoana ni yangu sababu mi ndo nainjoi kuliko wewe…one.

Nisher amejibu kwanini hakufanya hivyo kwa kusema:

“Mathematics zote hizo Mimi na team yangu pamoja na Ben Pol Tuliziwaza isipokuwa screen time ya Ben Pol isinge osha, kwa maana video hii Ilitakiwa Ku-inspire watu but at the same time isimame yenyewe na Ben Pol kama msanii.
Ndio maana nikaamua kuwa na story fupi kuonyesha Ben akiwa anapanda ngazi kwenye ghorofa lililo tupu, lina na ngazi nyingi sana hadi anakuja kufika juu kabisa na kuyaona mazingira katika namna ya tofauti, milima na mandhari mbali mbali. Halafu pia kama tungewaweka wahusika sikupenda niweke still pics manaa zimezoeleka. Nilitaka wawepo LIVE sasa Mathematics hapo nikuwapata wote sio kitu rahisi!! Unaongelea AWARD WINNING SUPERSTARS kwenye VIDEO moja sio mchezo, ingekua EXPENDABLES Movie HIYO….isingekua music video.”

2. Performances

Nimependa sana jinsi Ben Pol alivyofanikiwa kubeba hisia ya wimbo wake kwenye video hii. Ameitendea haki camera.

3. Production Design (props, costumes,sets, locations)

Nisher amefanikiwa sana kutafuta mandhari ya kuvutia na ya kawaida kabisa. Ule muonekano wa jumba linalojengwa, anapopanda ngazi, anapoimba akichungulia kwenye dirisha, sehemu ya vioo inayomfanya aone movements za nje nk viko poa sana. Kwa upande wa mavazi Ben kapendeza ile mbaya na ile miwani imemfanya avutie zaidi. Ule msalaba pia aliouvaa unaendana na ujumbe wa wimbo kuwa yote yanafanikiwa kwa kumwamini Mungu.

4. Visual Composition/ Cinematography (camera angles, camera,movement, lighting, framing of shots)

Linapokuja suala la kushoot angle mbalimbali za picha, Nisher ni monster. Nimependa sana jinsi alivyoweza kumchukua Ben Pol katika angle mbalimbali, za mbali, katikati, karibu na karibu zaidi (Extreme Close Up), Lean-Out na Lean in. Hata hivyo kama zilivyo video nyingi za Nisher, sijapenda mwanga wa video hii. Hiki ni kitu ambacho kama Nisher anataka kufanikiwa zaidi inabidi akifanyie kazi na asikilize ushauri anaopewa kuhusiana na suala hili. Angefanikiwa kuipa video hii mwanga na muonekano wa kung’aa zaidi, Jikubali ingeenda mbali zaidi.

6. Use of Audio Enhancements (sound and music)

Kwakuwa hakuna sauti nyingine inayosikika kwenye video hii zaidi ya wimbo wenyewe, hapa hakuna cha kuongea zaidi kwakuwa Jikubali ni wimbo uliotengenezwa kwa ubora mzuri, hongera kwa producer, Lucci kwa kazi nzuri.

7. Editing and Use of Visual Enhancements (Transitions, titles, credits, special
effects)

Hapa ndipo ambapo Nisher hakamatiki, ama hii ndio eneo la kujidai la Nisher. Jamaa ni mzuri sana katika uchanganyaji wa picha, muingiliano wa picha na mambo mengine. Hapa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

USHAURI

Ni wazi kuwa Nisher ametokea kukubalika mno Tanzania kwa uwezo wake lakini ni kitu kimoja tu kitakachomwangusha baadaye, MWANGA!! Ajitahidi sana kuondoa kasoro hiyo kwakuwa mwisho wa siku hata kama video ikiwa na creative shots, uchanganjaji picha na the best editing ever, haiwezi kufika popote kama ikiwa na GIZA.
Haya ni maoni ya watu wengine

Sydèricho DèJaysep

Kichupa kikali sema kwa ushauri mdogo broo badlika coz tumezoea sana kuona yho videos zna colour effects sana but other wise big up to you 99% men and also represent arusha man

Hamis Mwinjuma aka MwanaFA

Always count me in bruv..I like the concept,him alone..dope,nimewakubali

Dux Abdul Dugara

Nlikuwa si kukubalii kiivyo ila kwenyw dole ulini convice na hapa ndo umenimaliza kabisa mwanangu iyo video mi nafananisha na don judge me ya crissbrown we ni nomaaa sanaaa mzazi adamu juma ajipange

Fortune Ephata

Iko poa sana nimeipenda sana sana hii coz kwanza ipo kitofouti kidogo na video za kibongo maana tumeshazoea kuona majengo ya posta kila video inapotoka ila safi sana nisher unafanya vitu vizuri…one lv

Ben pol tangu aanze music hajawai kufanya video kali kama hii, dah umempeleka level nyingine nice video tishaaa sana


Source:Bongo5.com
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad