Lakini katika hali halisi, akina mama peke yao ndiyo wamekuwa wakiachiwa mzigo na majukumu yote ya kuwatunza na kuwalea watoto wao bila ushiriki wa kina baba. Na mara nyingi watoto hawa wanapogeuka na kuwa waasi na watukutu, lawama zote huwaendea akina mama. Ni jambo linaloudhi na kukatisha tamaa, tunapowaona akina baba wengi wakishindwa kuchukua na kuubeba wajibu wao kama ‘baba’ na viongozi wa familia ambao, watoto wao wanapswa kuiga mfano kutoka kwao.
Kwa kawaida, mtoto anakuwa ni jukumu la mama, hadi akiharibika au akinyookewa. Kama akinyookewa, baba hujifanya kwamba, yeye ndiye aliyehusika kumfanya mtoto awe hivyo, wakati hakuwa akijua alikuwa akisoma darasa la ngapi. Mtoto anapoharibika, baba huruka hatua nyingi akimlaumu mama kwamba, alimdekeza mtoto. Akina baba wengi wanaona kuwa, wajibu wa kuwatunza na kuwalea watoto wao, ni wa wake zao peke yao. Wao wanaona kwamba, wanao wajibu wa kutoa amri na kulaumu kuhusu malezi. Ni kama vile wao hawahusiki na watoto wao.
Hali hii ya kutojitambua na kutokubali kufanya marekebisho katika njia ya kufikiri na kutenda mambo na hasa yale yanayohusiana na watoto na familia kwa ujumla kwa upande wa wanaume walio wengi, imekuwa ikisababisha dhuluma dhidi ya wanawake wengi. Akina mama wengi pamoja na kukabiliwa na majukumu mengine ya uzalishaji mali, pia wamekuwa wakibebeshwa jukumu hili kubwa na zito la kuwatunza na kuwalea watoto wao, bila usaidizi kutoka kwa wanaume zao.
Jamii kwa upande mwingine imekuwa ikiwalaumu moja kwa moja akina mama kuwa, wamekuwa wakizembea na kuwadekeza watoto wao na kusahau kwamba, baba wa watoto hao wapo, lakini jamii haitaki kuwagusa wala kuwakemea……
Huo ndo utaratibu/utamaduni maana hata wahenga walisema asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.HAWAKUSEMA asiyefunzwa na babaye.....
ReplyDeleteKubali tu yaishe. Hio haina mjadala saaana japo haimaanishi kuwa baba hatakiwi kushiriki ktk malezi ya mtoto,hapana bali uhalisia ni kwamba mama anachukuwa sehemu kubwa mno ktk hili.
Labda ntoa hoja ameangalia upande moja tuu ukweli mama ndiye aneye kuwa karibu na watoto kuliko baba Utamsikia mama ana mwambia mtoto "Endelea na ujinga wako nitakuja kumwambia Baba yako" usemi huu anaulekeza kwa mtoto wakiume au kike wenya umri kati ya 5-10 wakati mama anweza kumuadhibu aje amwambia baba yake alafu baba yake naye akaziye kuwa kwake angepata kipingo zaidi lakini mama amemuadhibi hata mpinga. Mtoto akiona hayo atasema baba na mama ni kimoja. Lolilo baya kwa mama ni baya kwa baba lililo nzuri kwa baba ni nzuri kwa mama. Sivizuri siku zima mama lugha anayo itumia "nitakuja kumwambia baba yako" mtoto atakuwa kujua baba ndiye hataki hiki ila mama ana taka ila anogopa amri ya baba. Mtoto atakua akitafuta ndiya ya kumkwepa baba. wazazi tuwe pamoja kuwafundisha watoto llilo baya liwe baya kwa wote kama mumaamua mtoto hapingwa asile kwa siku ile na awe katika chumba mmoja asifanye jeuri ya kumptishia chakula dirishani. Muda muloa panga anaona munampa chakula tena munakula pamoja na huku wote mnasema maneno yakuonyesha kuwa yeye kama yeye mnampenda ilatabia yake. Mtoto akiona mama na baba kitu kimoja watoto wasiku hizi watasema "baba na mama noma sana" wakifikia umri mzuri wata washukuru sanasana
ReplyDelete