WIKI iliyopita kuliibuka sakata
zito lililochukua nafasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii, lililomuhusisha mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Hezelina
Mrema mkazi wa Mbezi Beach, eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam,
kuamua kuishi juu ya paa la iliyodaiwa kuwa ni nyumba yake.
Hatua
hiyo ilisababisha baadhi ya wanaharakati kujitokeza na kuahidi
kumsaidia mama huyo, aliyedai kuwa anataka kutolewa kwa nguvu ndani ya
nyumba yake halali, ambayo ameijenga na mumewe Samwel Opulukwa.
UKWELI WA MAMBO
Ukweli
juu ya suala hilo ni kwamba Hezelina hahusiki kwa namna yeyote na
nyumba hiyo, ambayo ni ghorofa moja, kwani imebainika kuwa si mke halali
wa Opulukwa na badala yake wana mahusiano ya kimapenzi.
Imebainika
kuwa mke halali wa Opurukwa alisha achana nae na mke wake huyo tayari
alishaweka pingamizi Mahakamani la kutaka hati ya nyumba hiyo
isibadilishwe mmiliki.
Mbali
ya Hazelina kutokuwa mke halali wa Opulukwa pia imebainika kwamba
mwanaume huyo aliitumia nyumba hiyo kuweka dhamana ya mkopo kwenye benki
ya TIB.
Imebainika
kuwa hatua ya Opulukwa kuweka nyumba yake dhamana ilikuja baada ya
rafiki yake ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Asasu Express Ltd kuhitaji
fedha za kuendeshea bishara yake, lakini alikumbana na kikwazo cha
kutakiwa kuwa na nyumba jijini Dar es Salaam, ambapo kwa kuwa hakuwa
nayo aliona amtumie rafiki yake huyo kufanikisha mkopo wake kwa
makubaliano kuwa ataulipa bila tatizo.
Hata
hivyo mmiliki huyo wa kampuni ya Asasu alishindwa kulipa mkopo huo wa
mamilioni ya fedha, ambapo benki husika ilianza harakati za kutaifisha
mali zake ili kufidia deni hilo, hata hivyo hazikutosha na ndipo
walipoamua kuiuza nyumba hiyo ya Mbezi Beach iliyopo kiwanja namba 235
Block D.
Imeelezwa
kuwa benki ya TIB ilimpa Opulukwa taarifa zote za deni husika pamoja na
kumpa Notisi ya kumtaka alipe deni husika ambalo ni 274,854, 256. 84
kutokana na rafiki yake kushindwa kulipa deni husika pamoja na mali zake
kutaifishwa.
Ili
kufuata taratibu za kisheria za kutaifisha nyumba ya Opulukwa, benki
hiyo ilitoa tangazo la kutoa tenda ya kuuza nyumba hiyo, ambalo
lilitolewa kwenye gazeti la serikali Januari 10,2011.
Hata
hivyo Opulukwa hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyosababisha benki
ya TIB kuipiga mnada nyumba hiyo na kufanikiwa kupata mteja, ambaye
aliinunua kihalali ikiwa ni pamoja na kubadilisha hati miliki ya nyumba
hiyo.
Jambo
la kushangaza Opulukwa aliendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo, TIB
ilifanya harakati za kumtoa kwa kuyatumia makampuni kadhaa ya udalali
ambayo yalishindwa kufanikisha kazi hiyo na ndipo Machi mwaka huu,
jukumu hilo la kumtoa Opulukwa lilipelekwa kwa kampuni ya udalali ya
Msama Auction Mart.
Baada
ya Kampuni ya Msama Auction Mart kufanya taratibu zake za kikazi na
kuridhishwa na uwepo wa deni husika, Juni 8, mwaka huu ilifika eneo la
tukio na kuanza kumtoa Opulukwa.
Hata
hivyo zoezi hilo lilikuwa gumu kutokana na baadhi ya maofisa wa Polisi
wa Wilaya ya Kinondoni kuingilia kati, ambapo waliitisha kikao cha
pamoja kati ya maofisa wa kampuni ya Msama Auction Mart na Opulukwa,
ambapo maamuzi yalikuwa ni kusimamisha zoezi hilo hadi pale mkopaji huyo
atakapopata baraka za Mahakama juu ya uhalali wa kuendelea kuishi
kwenye nyumba hiyo.
Baada
ya maamuzi hayo ya jeshi la polisi, Opulukwa alifungua kesi ya madai ya
kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa vifaa vyenye thamani ya shiringi 195
milioni, jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.
Juni
11, mwaka huu mara baada ya Opulukwa kukosa vielelezo vilivyompa
uhalali wa kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo kama alivyoagizwa na
Mkuu wa Polisi wilaya Kinondoni, kampuni ya Msama Auction Mart
iliendelea na zoezi la kumuondoa.
Wakati
maofisa wa kampuni ya Msama Auction Mart wakiwa na uhakika wa
kukamilisha zoezi lao pamoja na kuondoka eneo hilo,ghafla walipigiwa
simu na walinzi walioachwa kwenye eneo hilo kuwa kuna mtu yupo ndani ya
nyumba, ambaye inaelezwa aliruka ukuta ili kufanikisha lengo lake.
Hatua
hiyo ya Hazelina iliwashangaza maofisa wa Msama Auction Mart, ambao
walichukua jukumu la kupiga simu polisi ili kuhakikisha mama huyo
anaondolewa kwa njia ya amani na utulivu.
Wakati
huo tayari Hazelina alikuwa ameshapanda juu ya paa la nyumba hiyo, huku
akitishia kujirusha ili kuutoa uhai wake endapo angetolewa kwa nguvu.
Aidha
alikwenda mbali zaidi kwa kuvua nguo ili kuonesha utupu wake, lengo
lake likiwa ni kutowapa nafasi walinzi wa kiume kutomsogelea.
Hatua ya mama huyu kuonesha utupu wake na kuendelea kukaa juu ya paa la nyumba hiyo ilizua maswali na kuwafanya baadhi ya waandishi wa Habari kufika eneo hilo ili kujua ukweli wa mambo.
Kutokana na kauli za uongo za mama huyo, alifanikisha kuwaaminisha waandishi wa habari kuwa kuna hila zinafanyika ili kupora nyumba yake, ambayo alidai kuwa ni halali yao.
Hata
hivyo maamuzi ya mama huyo kuendelea kukaa juu ya paa la nyumba hiyo,
yalidumu kwa muda wa siku mbili, ambapo Juni 13, mchana kwa hiyari yake
aliamua kushuka baada ya kumuona jamaa yake akiwa ameshikilia karatasi
zilizodaiwa kuwa zimetoka Mahakama ya Kinondoni.
Uchunguzi
wa wetu umebaini kuwa Opulukwa hakumueleza ukweli mama huyo,
ambapo ukweli halisi wa zoezi zima la kuhamishwa kwenye nyumba hiyo
analijua.
Aidha
imebainika kuwa mwanamama huyo si mke wa Opulukwa, kwani mke wake
halali anajulikana kwa jina la Rachel Paulo Ng’wahi, amabaye ndiye
aliyefungua kesi ya kupinga hatua ya mume wake kutumia nyumba yao
kumuwekea dhamana ya mkopo rafiki yake ambaye ni mmiliki wa kampuni ya
Asasu.
Ukweli
ni kwamba benki ya TIB na kampuni ya Msama Auction Mart, walikuwa
sahihi kumuondoa Opulukwa kwenye nyumba hiyo, hakuna sheria yeyote
waliyoivunja na hawakuwa na nia ovu ya kutaka kumpora mama huyo na
Opulukwa aliyedai kuwa ni mumewe nyumba kama alivyodai kwenye vyombo vya
habari.
Credits:Mpekuzi