Mwanza. Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani
Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop
zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya
wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM).
Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye
mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10,
mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza,
Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na
kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi
zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi,
moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa
vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo
ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu
alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba
laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM
lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.
Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari
ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na
maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza
kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.
Kwa maovu haya na mengine mengi. Ukiona mtu anashabikia ccm hasa akiwa chini ya miaka 40 hivi jua ana matatizo ya akili. Wametunyima elimu bora ili watutawale.... wa tz semeni ccm basi.
ReplyDeleteAcha siasa ww toa comment kutokana na mada sio unaleta siasa kwa kila jambo usilete uccm na uchadema na ucuf humu chambua mada tujue wapi kuna tatizo
ReplyDeleteKwanza mkuu wa kituo awajibike!polic waliokuwa zamu pia wawajibishwe haraka iwezekanavyo!
ReplyDelete