AIBU TENA:COMPUTER ZA USHAHIDI ZILIZOTUMIKA KWENYE UWIZI WA ATM ZAIBIWA NDANI YA KITUO CHA POLISI

Mwanza. Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM).
Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.
Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa maovu haya na mengine mengi. Ukiona mtu anashabikia ccm hasa akiwa chini ya miaka 40 hivi jua ana matatizo ya akili. Wametunyima elimu bora ili watutawale.... wa tz semeni ccm basi.

    ReplyDelete
  2. Acha siasa ww toa comment kutokana na mada sio unaleta siasa kwa kila jambo usilete uccm na uchadema na ucuf humu chambua mada tujue wapi kuna tatizo

    ReplyDelete
  3. Kwanza mkuu wa kituo awajibike!polic waliokuwa zamu pia wawajibishwe haraka iwezekanavyo!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad