Anaweza asiwe na hit redioni kwa sasa lakini Ali Kiba ndiye msanii wa Tanzania ambaye nyimbo zake zinasikilizwa zaidi mjini Muscat, Oman, kwa mujibu wa Mtanzania aishiye huko.
Bongo5 ilikuwa ikichat leo na Mtanzania huyo, Rayya Al Habsi. Ameiambia kuwa muziki wa Bongo Flava unasikilizwa mno nchini humo hata na watu wasiojua kabisa Kiswahili.
“Bongo fleva muscat inapendwa sana, ninafahamu wengi ambao hawafahamu Kiswahili lakini kwenye magari yao wanapiga nyimbo za Ali Kiba, amesema Rayya.
Mbali na Ali Kiba, amesema wasanii wengine wa Bongo Flava wanaopendwa ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz na Dully Sykes wengine wanapenda zaidi mduara kama nyimbo za Kilimanjaro Band, AT na Off Side Trick.
“Ukija kwenye band Twanga Pepeta imekuja huku mara nyingi na show zao zilikuwa Muscat Festival.”
Ameongeza kuwa wasanii wa Tanzania wanaofanya hip hop hawana umaarufu kama walivyo waimbaji nchini humo.
“Sina hakika kuhusu hip hop japo nakumbuka wakati wa kina GK na AY watu walikuwa wanasikiliza nyimbo zao. Hapa muscat wengi wanapenda nyimbo rahisi kufaham na lugha imetumika ni ya kawaida. Sasa mziki wa kuimba ni rahisi kuusikiliza,” amesema.
Mwezi ujao TID anatarajiwa kwenda kufanya show mjini Muscat.
Source:Bongo 5
Hilo kweli kwani Mimi na family yangu huwa takusikiliza sana kwani hata watoto wangu wampenda sana Ally kiba
ReplyDeleteHuyo ndo Ally k big up
ReplyDelete