RIYADHI, Saudi Arabia
JAMAA mmoja amemuuza mwanae wa kumzaa kutokana na matatizo ya kifedha aliyonayo.
Saud bin Nasser Al Shahry, raia wa Saudia Arabia aliweka picha ya
mwanae huyo wa kiume kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii ‘Facebook’
akimnadi kwa bei ya dola milioni 20.
Baba huyo alidai kuwa kitendo cha kumuuza mwanae ndiyo njia pekee ya
kuondokana na maisha ya kimaskini aliyokuwa nayo kutokana na madeni.
Mahakama ya nchini humo ilifunga biashara yake ya kukusanya madeni
isiyo rasmi aliyokuwa akiifanya ili kujikimu kimaisha, hivyo alibaki
hana mbele wala nyuma hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha.
‘Mfanyabishara’ huyo alidai aliomba Serikali imsaidie fedha, lakini
ilimkatalia kwa kuwa umri wake ni zaidi ya miaka 35 ambao ni mdogo.
Alisema akifanikiwa atatumia fedha hizo kumtunza mke wake na mwanae
mwingine wa kike.