Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu
nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa
watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
Takwimu
hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha
kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati
asilimia 51.68 ndio wazazi halali.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa
Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria
Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Dar es Salaam.
Ingawa hakutaja idadi kamili ya
waliojitokeza kupima DNA, alisema idadi hutofautiana mwaka hadi mwaka.
Ili kufanya vipimo vya DNA, wazazi hulazimika kulipia Sh 100,000.
Machuve alisema kazi ya DNA si kutambua watoto halali na wasio halali pekee, bali vipimo hivyo vina umuhimu mkubwa kwa jamii.
Alitoa
mfano kuwa, matumizi ya Teknolojia ya vinasaba vya binadamu yamewezesha
kesi mbili za mauaji ya vikongwe na albino kutolewa hukumu katika mikoa
ya Shinyanga, Kagera na Sumbawanga baada ya kufanyika kwa uchunguzi
katika matukio manane.
Aidha, alisema katika majanga mbalimbali
yaliyokumba nchi ikiwa pamoja na milipuko ya mabomu yaliyotokea Mbagala,
Dar es Salaam mwaka 2010 walitambua mabaki ya askari sita ambao baadaye
walichukuliwa na ndugu zao na kuzikwa.
Alitolea pia mfano wa tukio
la moto katika Shule ya wasichana ya Idodi mkoani Iringa ambako licha ya
kuungua vibaya, miili ya wanafunzi 12 ilitambuliwa hivyo makaburi yao
kutambuliwa. Katika Jengo la ghorofa lililoporomoka mtaa wa Kisutu mwaka
huu, marehemu 23 walitambulika.
Aidha, katika ajali ya Ndege ya
Comoro mwaka 2010 mabaki ya miili ya marehemu 25 ilitambuliwa huku
katika masuala ya uhamiaji teknolojia hiyo ilitumika kudhihirisha hawana
uhusiano na wananchi wa Tanzania.
Machuve alisema katika masuala ya
ubakaji na mimba za utotoni teknolojia hiyo imesaidia kuwa fikisha
wahusika mahakamani pamoja na katika wizi wa kutumia silaha.
Kichwa cha habari, kinapitosha! Si kweli Kama ukichulia wanaume wote wenye watoto Tanzania nzima! Hii takwimu inawahusu wale wenye mashaka Kama watoto ni wao au la! Sasa mtu akishakua na Shaka lazima kutakua na dalili alizoziona...
ReplyDelete