AZZAN:NITAJIUZULU IKIBAINIKA NIUZA MADAWA YA KULEVYA

MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan. Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.

Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha.

“Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo.

“Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.

“Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernad na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.

“Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu,” alisema Azzan.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni,” alisema Azzan.

MTANZANIA ilipomuuliza kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, alisema atakachokifanya anamuachia Mungu.

“Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua,” alisema Azzan.

Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa kupitia mitandao, ziliripoti kukamatwa kwa Watanzania wawili nchini China wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Dola milioni 3.34 za Marekani.


habari NA BAKARI KIMWANGA, MOSHI
chanzo - Mtanzania
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah, mbunge wangu...sina cha kusema zaidi ya: inawezekana ni siasa za kuchafu
    ana. nimesoma ile barua nimepata maswali kibao. kuna sehemu inasema vigogo wako wengi, lakini ametajwa mmoja tu Idd Azan, halafu mwandishi hajaweka anwani, (labda kwa sababu za kiusalama), inaonekana kunamashaka na chanzo hiki cha taarifa. VERDICT: nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na katiba. presumed innocent untill proven guilty without reasonable doubt. haki itendeke. please verify the source, tusifanye hivyo mana itafikia mahali mtu akijisikia kukuchafua tu anaandika barua yake na shutuma zzake anasambaza. na hivi hizi blog zisivyokuwa na usimamizi...mhhhhhhhh...sitaki kufikiria jinsi watu watakavyochafuana. mwisho ni watu kuumizana. tuwe makini ndugu...

    ReplyDelete
  2. Hii biashara ni hatari sana na tena ukwa mshabiki wa kufatilia ni kina nani wanahusika walahi utauliwa kabla ya siku si zako. mm namfahamu dada mmoja mumewe alikuwa ni punda. basi kila siku safari za uingereza na australia. basi mwanaume alikuwa ana hela huyo acha. nikimuuliza dada yangu shemeji anafanya biashara gani dada yangu ananijibu anauza batiki a mashati ya vitenge ulaya. mm nasema moyoni moyoni mmh haiwezekan. kwan hata mwaka ulipita siku akasafiri kwenye biashara yake ya mashati ya vitenge na batiki. wenzake wasipige simu australia. wakakamatwa na wako nadi hadi leo hiyo ilikuwa 2010 mwanzoni. basi huku kwa dada yangu acha aanze kutapatapa. kila siku nyumbani kwake wanaenda mapolisi. wengine si mapolisi wengine ni wezi. siku moja nakwambia akapigiwa simu na mtu asiye mjua. akamuuliza una shida gani? basi dada yangu akasema shida yake. yule jamaa asiyejulikana akamwambia dada yangu ammpe account number yake akienda bank atakuta hela na hizo hela akishazipata asimtafute tena na wala asiwe na wasiwasi mumewe atatoka tu na akaambiwa ile simu card aidestroy. basi dada yangu akafata maelekezo kesho yake kweli kwenda bank akakutana na kitita chake. kwa hiyo ndugu zangu hii nchi ishaliwa. tunaongozwa na mafisadi na wauza madawa ya kulevya. ww unafikiri Lowassa anapata wapi hela za kutoa misaada kila leo? mm ndiyo maana huwa najisemeaga watanzania waliobahatika kuwa nje ya nchi wakawa na maisha yao wakakae hukohuko hata kama unachamba vibibi au unabeba box mara mia kuliko kuja nchi watu wanajidai ooh mali asili nying wakati wanafahidi wachache wenye roho za tamaa ambao hawaridhiki. basi ibene aau fanyeni hayo mauza mauza tengenezeni barabara, rekebisheni miundo mbinu ya maji hata umeme. tumieni hizo hela haramu na za wivu kufungua biashara na muajiri vijana wanaotangatanga mitaani. basi mnajikusanyia hela kwa uchoyo na ubinafsi uliopitiliza. utafikiri hamna watoto. ILA ALL IN ALL KARMA IS BITCH. Kama haitakukumba ww jua kwa njia moja ua nyingine kizazi kitalipa tu. VIONGOZI MBULULAS WA TANZANIA. very stupid utafikiri wakienda ulaya na amerika sijui hawaoni hayo maendeleo ya wenzetu mm nachukia sana.

    ReplyDelete
  3. Kama kweli amekusingizia kukutaja jina mbona akutaja wengine kakutaja wewe...na kama si kweli basi lazima utakuwa unahusika kwa njia moja au nyingine..mnatumia majina ya uheshimiwa kwa manufaa yenu binafsi wakati wananchi wa kawaida ana ata uhakika wa mlo wa siku moja..inatia hasira na inasikitisha kuona viongozi wa nchi ambao ilibidi wawe mstari wa mbele kukemea biashara ya madawa ya kulevya lakini wao wenyewe ndio wafanyaji wakubwa wa biashara hizo,Vijana wanazidi kuharibika mitaani na madawa ya kulevya na hii inatokana na kukata tamaa ya maisha sababu viongozi wetu wanajinufaisha maslai ya nchi kwa faida zao binafsi...Swala hili ata mi limenigusa kutokana na mdogo wangu ambae alikuwa na muelekeo mzuri wa maisha yake laki sasa amejiingiza ktk utumiaji wa madawa ya kulevya na amelost kila kitu alichokuwa nacho na mi binafsi nilitumia pesa nyingi kumsomesha mpaka chuo lakini leo all for nothing....Lakini pamoja na kutajwa ata majina yao hakuna sheria yoyote itakayo chukuliwa sababu Viongozi wakubwa ndio wafanyaji wa biashara hizi na hao POLISI ndio sitaki ata kuwaona wala kuwasikia sababu wao ndo Washiriki wakubwa wa haya yote na wanawajua wote wanaofanya biashara hizi ata Kuna mtoto wa kigogo wetu wa nchi nae anafanya biashara hizi mpaka raia wa kawaida wanajua inakuwaje polisi wasijue..We Azzan usitufanye si wajinga kuconfuse watu we unafanya kweli biashara za madawa ya kulevya na ni afadhali uwataje wenzako pia..Na nyie polisi endeleeni amjui kuwa watu tumeshachoka na manyanyaso,uonevu,na kufanya wajinga..Nakwambieni nyinyi na STUPID viongozi wenu uko tunakokwenda mtaona na itakuja tuu..Manaake naona ni kheri wananchi tushike mabunduki sasa alafu tukose wote kwanini mnajinufaisha nyinyi tu na familia zenu kwani si sio watanzania na nchi sio yetu sote..Haya tutaona

    ReplyDelete
  4. POLISI sita wanamfuata wema sepetu kwaajiri ya kumtukana mtu..Sasa na Majina pia mmesaidiwa kupewa wanaofanya biashara za madawa ya kulevya nyie si mnajifanya amuwajui sasa tuone mtafanya nini..PUMBAVU ZENU

    ReplyDelete
  5. Maji yashamwagika kamata aliyetajwa weka ndani atawataja wenzie,akiendelea kuwa uraiani ataficha ushahidi huyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo umeongea kaka..lakini hao Polisi wenyewe ndo deal zao basi atakamatwa mtu hapo,ingekuwa mimi au wewe tiyari zamani tushawekwa ndani lakini bwa.mheshimiwa basi watakwambia uchunguzi unaendelea ili wawasaurishe watu na ndio ishu ishapotelea mbali kwani POLISI+VIONGOZI wa kibongo atuwajui HIZO NDO ZAO watafanya hilo deal wapate rushwa ya maana..na kama amjui nyie polisi hamna imani tena raia na amuaminiwi kabisaaa na kitu kizuri tunawajua vizuri mpaka akili zenu kuliko mnavyojijua wenyewe...Jamani mi sijawai kusikia nchi yoyote ile eti majambazi wanakwenda kupola kituo cha polisi za hapa kwetu bongo sasa utasema kuna polisi hapa na usikute wao wenyewe wanajifanya wameingiliwa kumbe wanataka kupoteza ushaidi wa mtu sababu hili tukio la polisi kuvamiwa ndani ya kituo chao mi sijawai kusikia kabisaaaaa..Lakini ngojeni tu siku itafika na sisi raia wa nchi tutawaonyesha kuwa tunanguvu zaidi yenu na hii nchi ni ya kila raia kwa haki sawa na si kama mnavyofanya kama nchi ya Mafisadi wenu serekalini..WAPUMBAVU MSIO KUWA NA HAYA KILA KUKICHA

      Delete
  6. Alafu nyie mnaemtetea najua ukweli uko wapi au ndo kujipendekeza kwenyewe na kama na nyie ndo biashara zenu pia basi nyamazeni kimya kabla mizuka isipande hapa,,NOSENSE

    ReplyDelete
  7. mnajitengenezea pesa za kustarehesha nafsi zenu kwa kuangamiza vijana wenzetu mnawafanya punda wengine ndio wateja, wanapiga debe na kuteseka mwisho wa siku hana hata mia keshajidunga mnatunisha mifuko kwa kunyonya uhai wa wenye kutafuta kilevi cha kuondoa stress za maisha ya bongo. Kama ni kweli mheshimiwa unahusika japo hata mimi nina zambi KAMA BINADAMU ila ntakua wa kwanza kurusha mawe

    ReplyDelete
  8. Mapovu yanawatoka wenzenu wanakula baytaaaa

    ReplyDelete
  9. Katika historia ya madawa ya kulevya ukifuatilia kwa undani unakuta yalianza kuingizwa na kupitia nchini miaka ya 80 huko.Lakin kwa sababu wafanya biashara hii ni vigogo kila mara ilitolewa taarifa watuhumiwa wameitoroka polisi airport.Ikawa ndo kukomaa kwa biashara haramu hiyo.Kwanin wasinyongwe kama inavyofanya CHINA?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad