BAADA YA JOYCE KIRIA KUSHAURIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA NA HII NDIO KAULI NA MSIMAMO WAKE

Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote
 My Hubby Henry Kilewo.
 My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.

 Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama)
 Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"

Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.


Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????

Fans Wangu wote naamini mtakuwa mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu, Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE 

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rashid Ramadhan7 July 2013 at 10:46

    "Kama ningekuwa na mamlaka ya kumwamuru binaadam kumwabudu binaadam mwingine,ningemwamuru mwanamke kumwabudu mumewe" Hayo ni maneno kutoka katika kitabu kitakatifu cha mwenyezi mungu QURAN tukufu na yalisemwa na Mtume Muhamad SAW. Uko sawa JK kumsuport mumeo hata kama ukikosa suport ya binadam usijali hao binaada hukuzaliwa nao na hutakufa nao zaid tu zidisha maombi kulingana na imani ya dini yako na usichanganye mambo.!

    ReplyDelete
  2. Yana mwisho dada yetu, wako wapi watawala wababe karibu afrika yote? Kenya Kenyata, uganda Idi amin, congo mobutu na hata historia inaobyesha hivo. Polisi kumkamata mtu ni tuhuma hukumu hutolewa mahakamani sijui kwa nini polisi wetu wanaficha ficha, wanamfanya mtuhumiwa kaisha hukumiwa!, na hata kama kahukumiwa familia yake ndo ya kwanza kutaarifiwa. Nwisho wa kuwatisha na kuwaogopeaha
    watz unakaribia na siku wakisema basi risaisi zitawaishia na tz imara itabaki. Endelea kumsuport
    mumeo dada. Nashauri mtu akituhumiwa akamatwe
    kwa haki na sheria, mahakama itachambua na kutupilia
    mbali pumba za polisi maana siku hizi kila mwana
    siasa wanataka wamshitaki kwa kesi ya ugaidi.. kazi
    ipo.

    ReplyDelete
  3. Ukimpiga chura teke umemuongezea hatua.Kilewo na Lwakatare wamepata umaarufu ambao hauna bei .ccm inajidanganya eti itaimaliza chadema kumbe ndo wanaifagilia bila kujijua.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad