Kiswahili hiki cha waswahili ni kama mwanaharamu huko pwani ya
waswahili, masikini kimezaliwa wakati mama anajifungua akafa, kikalelewa
na baba wa Kambo mwalimu Nyerere naye kwa kansa ya damu akafa.
Kiswahili aliachwa mdogo lakini mwenye afya njema akiendelea kukua,
hongera kwa baba wa kambo ambaye kweli alimpenda kiswahili japo alimuua
mke wake wakati akizaliwa. Kiswahili yatima ambaye sasa anabidi akue
mtaani tena aitwe mtoto wa mitaani maana hata kanyaga tena ikulu wala
hafla za kimataifa, labda Chissano alirejee kwenye madaraka huko nchi ya
jirani Msumbiji. Hongera Chissano kukumbuka kiswahili japo TZ ulipita
tu kuomba msaada wa kukomboa nchi yako, jasiri hakuacha kusahau mchango
wa Kiswahili kufanikisha mambo ya Wamsumbiji.
Kwa nini tumeshindwa kutumia fursa nyingi ama zote kukistawisha
kiswahili, lile baraza la kiswahili linakula tu fedha za watanzania au
linafanya kazi gani??? halikumshauri hata rais kutumia fursa ya ujio wa
obama kutangaza kiswahili?? au rais alikaidi?? rais si ni taasisi au huu
utaasisi ni majibu ya kijanja janja kule kwa Makinda ANNE??? Hongera
Kenyairways kututangazia Kiswahili duniani.
Kwa nini rais ataabike kiasi kile kuongea kiingereza wakati kiswahili
kipo? hata kama rais angekuwa mzuri sana kwa kiingereza Je haikuwa fursa
ya kutangaza utaifa wetu na kiswahili chetu?? hivi wajapan, wachina,
warusi na waarabu wakiongea lugha zao ni kwambma hawajui kiingereza
kabisa, au wanataka kuweka alama sahihi juu ya wao ni kina nani,
kujitambulisha kwa dunia kuwa ni mataifa huru yenye lugha zao huru kwa
matumizi yao. Kiswahili umekosa mvuto huo nyumbani na ugenini. pole haya
yote yanamwisho, ama siku ukijifia au siku ukikumbukwa fedheha kilemba
cha ukoko.
Kweli watanzania mmetutenda tena sana, fursa moja ikipotea mikononi na
mdomoni mwa ikulu, hi hatari sana maana inaweza isije tena kwa miongo
kadhaa, washauri wa rais, ikulu mnafanya nini??? mnashauri nini?? mbona
imekuwa kama mnamkomesha rais? aliwakosea nini sasa mnamlipa ubaya wote
huo?? si aliwaaamini mmsaidie kazi?? Kwani kiswahili kitaongewa na nani
kama sio rais na ikulu ya dar??? mtoto kiswahilil kakosa nini hadi
anakataliwa kwao???
Naomba serikali ifikirie tena pengine iweke mikakati kuwa rais na ikulu
waongee kiswahili kwenye shughuli zote zikiwemo za kimataifa, ipo siku
aibu itakuwa kubwa, narudia hii tunaona ni harufu tu, ipo siku tutaona
mzoga wenyewe.
Kiswahili Kiswahili nakupenda lugha ya taifa langu.
Naomba kuwasilisha.
Source
Kweli inasikitisha kwanini hatutumii kiswahili sehemu muhimu kama hizi. nilimchek first lady akisoma hotuba kwa ngeli ile pronuotiotions yake daah! kuongea kiswahili ktk mikutano sio kujidhalilisha ila itaonesha tunajali utamaduni wetu.
ReplyDeleteKweli inasikitisha kwanini hatutumii kiswahili sehemu muhimu kama hizi. nilimchek first lady akisoma hotuba kwa ngeli ile pronuotiotions yake daah! kuongea kiswahili ktk mikutano sio kujidhalilisha ila itaonesha tunajali utamaduni wetu.
ReplyDelete