HALI YA MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE AKIWA HOSPITALINI SOUTH AFRICA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI.

MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka. Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki. Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua. Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni. Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MANGE KIMAMBI NEXT

    ReplyDelete
  2. Nenda states ukafanyiwe plastic surgery si una mawe

    ReplyDelete
  3. Tumekua kama manyama

    ReplyDelete
  4. Tumekua kama manyama

    ReplyDelete
  5. Hyo thuluma au katembea na mke wa mtu!

    ReplyDelete
  6. Get well soon,,

    ReplyDelete
  7. Binafsi nasema pole kwa maumivu Kibinadamu, ila kwa yaliyomo humu sidhani kama unastahili pole ya aina yoyote Kweli usilo lijua ni sawa na usiku wa giza. Sikujua Mengi kuhusu wewe na sasa nimesoma, nimefikiria na kujua. Ibaki kuwa pole kama binadamu lakini U-Mtu mbaya kwa taifa langu na jamii yangu. http://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/66439-serikali-imewekwa-mfukoni-na-said-na-ghalib-saad-wa-home-shopping-center.html

    ReplyDelete
  8. haki haki haki huinua taifa. Tusipokuwa na uhakika wa kupata haki tunazitafuta wenyewe. Hiki ni kisasi wala hakuna uonevu hapa. Ni muonevu kaonewa. Pole sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad